Tulonge

T.I asababisha 'mzubao' kwa binti yake katika pati la Birthday yake!

Limefanyika pati la nguvu pande za huko majuu lililohusiana na sherehe za kuzaliwa kwa Zonnique.Zonnique ni binti kipenzi wa T.I.Katika pati hilo lililoshiba na la nguvu, baba yake na Zonnique,yaani:


T.I, alimsuprise binti yake huyo kwa usafiri wa maana aina ya "Porsche" ikiwa ni zawadi rasmi ya yeye kufikisha umri wa miaka 16.


Familia ya T.I na Tiny imeshuhudiwa ikiwa katika wakati nyeti wa furaha,wakifurahia birthday ya binti yao Zonnique.

Katika sherehe hizo wamehudhuria pia wakali wa kufoka foka katika mike wa huko pande za juu.Miongoni mwa waliohudhuria  katika pati hilo ni mkali:
Nelly,Christian Combs,Lil Wayne akiwa na binti yake Reginae,Diggy Simmons, na Misa Hylton Brimm.

Zoninique alionekana akiwa amebebwa katika kiti cha enzi utadhani binti mfalme wa Misri.

T.I ana watoto sita,mkubwa wao akiwa Zonnique.Hii ina maana Mr.T.I  atafanya mengi zaidi kwa watoto wake wengine watano pindi watakapofikia umri huu wa miaka 16.

Na Chalii a.k.a_ILYA

Views: 670

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ANGELA JULIUS on March 29, 2012 at 8:21

@ Manka kwa kweli mimi nimesema nitamtengenezea cake yenye gari expensive more than all in the world kuhusu kununua kavukavu huko sipo mwenzangu ha ha ha ha wee waache tuu dismas na mwenzake Chalii waende kupasuka msamba

Comment by ILYA on March 28, 2012 at 23:12

Itabidi Chalii mimi  nianze kuzichanga na kuziweka mdogo mdogo  kwenye kibubu changu kwa ajili ya kabinti kangua kapenzi,ili the day kanagonga kwenye miaka 15-16-17...nakasuprise kwa BENZ LA BMW.!

Hilo linawezekana, siwezi kushindwa na nyuki bwana!!,maana Mheshimiwa Nyuki anaanza taratibu taratibu kujenga mzinga wake,kisha linatoka bonge la mzinga wa nyuki uliojaa asali kibao.

Comment by Alfan Mlali on March 28, 2012 at 18:40

Duh..watu wanafanya mambo makubwa sana kwa jeuri ya pesa. Sisi wengine hata hatukumbuki birthday za watoto wetu...Msiba huu.

Comment by manka on March 28, 2012 at 17:57

amina bandugu, @ angela na dismass nyie timizeni tu ahadi haswaa dismass kama nitakuwa hai nitakukumbusha.

Comment by ANGELA JULIUS on March 28, 2012 at 16:22

NAMALIZIA KWA KUSEMA AMEIN

Comment by Tulonge on March 28, 2012 at 16:15

Hahaahhahaaaa Angela hiyo ndoto yangu lazima itimie katika jina la Yesu.

Comment by ANGELA JULIUS on March 28, 2012 at 16:10

HA HA HA TULONGE HATA BAISKELI HUNA MDOGO WANGU LOL ILA NI VEMA KUOTA NDOTO KAKA HATA MIMI NITAMNUNULIA CAKE YA GARI.

Comment by ILYA on March 28, 2012 at 14:40

hahaha,tulonge umenichekesha sana!

Comment by Tulonge on March 28, 2012 at 14:11

Naona jamaa ameonesha upendo mkubwa kwa mwanae. Sijui siku ya birthday ya baby wangu nitamnunulia nini? Nways, nitamchukulia V8 itamtosha teh teh teh teh

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*