Tulonge

Tafadhali msaidie mtoto Zuberi M. Zuberi apone ugonjwa huu

Assalaam Alaykum.

Kufuatia kichwa cha habari kilichopo hapo juu, nachukua fursa hii kutoa Historia fupi ya Kijana huyu anako toka na jinsi ugonjwa alionao ulivyo gundulika mpaka hivi sasa.

Zuberi Mgeni Zuberi alizaliwa Mwaka 1995 katika Kijiji cha Kwale Kata ya Kwale Wilaya [mpya] ya Mkinga Mkoa wa Tanga. Alifanikiwa kumaliza Shule ya Msingi kwenye Kata yake hiyo na akabahatika kuchagulia Mwaka 2010 kuendelea na Masomo ya Sekondari ambayo ipo kwenye kata hiyo. Lakini hakuweza kuendelea na Masomo hayo kwa ajili ya Ugonjwa huo. Mwandishi wa habari hii ni Ndugu wa karibu wa Mama yake Zuberi.Bado wanaishi pamoja na Baba mzazi wa Zuberi hadi leo na jina lake ndilo hilo Mgeni.

Shughuli wanazofanya ni uvuvi na ukulima mdogo. Kipato chao ni cha hali ya chini kiasi wali shindwa kumfanyia uchunguzi Kijana wao ili wafahamu ni kipi kinacho msumbua Mtoto huyo ambaye mara kwa mara alikuwa akisumbuliwa na Tumbo hivyo kufikiria kuwa ndiyo Maradhi yanayo msibu, kwa hiyo walikuwa wa
kimpatia Dawa za Tumbo ambazo hazikua zikitoa nafuu ya moja kwa moja na ilibidi awachishwe kundelea na Masomo ya Sekondari ndipo hapo Mwandishi wa Habari hii ambaye wakti huo alikuwa akiishi Kisiwani Pemba kwa shughuli za Ujenzi wa Barabara alipo fahamishwa na akatoa msaada wa ushauri na fedha ili Kijana apelekwe kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bombo Mjini Tanga kwa Uchunguzi na tiba husika mwaka 2011, mwezi Juni.

Hapo ndipo alipo gundulika kuwa anasumbuliwa na Ugonjwa ndani ya Moyo wake hivyo Hospitali hiyo ikampa Rufaa ya Kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amekuwa na Kliniki hadi leo. Cha kusikitisha ni kuwa Madaktari wa Hospitali hiyo wameshindwa kumpa Rufaa ya kwenda Nchi za nnje kwa Matibabu kamili baada ya wao kutokuwa na vifaa au ujuzi wa tiba hiyo, hivyo ilibidi kutafutwa njia nyengine kwenye Hospitali Binafsi ikiwemo Regency ambao baada ya utafiti wao wakasema anahitajika kwenda India kwa Matibabu na Gharama kwa kipindi hicho zilihitajika wastani wa Dola 6,000 za Kimarekani sawa na Shs. 9,600,000/= za Tanzania. Zikipatikana anaweza kusafirishwa na msaidizi wake mmoja.

Maelezo Mengine kwa kina yana weza kupatikana kwa kuwasiliana na Mwandishi wa Habari hii [Mjomba] moja kwa moja kwa kutumia nambari zifuatazo:- 0777 980492 au 0714 980492. Jina lake ni Bwana Yunus Ally Chui na mshirika wake wa karibu ni Bwana Feisal Y. Chui Nambari yake ni 0773 449662.

Msaada wa kifedha unaweza kutumwa kwenye akaunti zifuatazo: 5753735527 kwa Fedha za Kitanzania na 5753735502 kwa fedha za kigeni Bank ya Exim tawi la Tanga kwa Jina la Yunus Ally Chui.

Ina ambatanishwa kwenye Barua hii Picha ya Zuberi ili kuthibitisha namna gani Ugonjwa huu ulivyo mbadili Umbile lake.

SHUKRAN

Yunus Chui.

via: wavuti.com

Views: 649

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Grace Kamonga on September 23, 2013 at 0:00

Nimeumia sana kwa tatizo lake. Ila najua atapona ikiwa atakuwa na imani, Nashauri aende kwa Mchungaji Nabii malisa B, G. au Mchungaji Jeremia yuko mbagala ambaye hata madaktari wa hospitali wanamwomba ashughulikie masuala magumu yaliyoshindikana hospitali.  wengi wamepona kwa hawa watu wawili ni wachungaji waenye upako wa ajabu sana

Comment by KUNAMBI Jr on September 5, 2013 at 8:29

Duuh Mungu atulinde

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*