Tulonge

Tanzania yashauriwa kujiondoa ktk mchakato wa uundwaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki

Baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi wa dini, wanasiasa wasomi na wataalamu, mkoani Mbeya wameitaka serikali ya Tanzania kujiondoa katika mchakato wa uundwaji wa shirikisho la Afrika Mashariki kutokana na mizengwe inayoonyeshwa na baadhi ya viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wakizungumza kufuatia kauli ya Waziri wa Afrika Mashariki, SAMWELI SITTA bungeni, wananchi wamesema kujiondoa katika mchakato huo hakutaiathiri Tanzania ambapo Mwenyekiti wa asasi ya wasomi na wanataaluma mkoani Mbeya, PRINCE MWAIHOJO amesema Watanzania wanapaswa wakumbuke kuvunjika kwa Jumuiya hiyo mwaka 1977 ambako kulisababishwa na mmoja wa marais wa nchi wanachama.

Mchungaji DAUD KATULE wa TAG, mchambuzi wa masuala ya siasa mkoani Mbeya DAIMON MWASAMPETA na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR – Mageuzi jijini Mbeya EUGEN KISONGA wametoa maoni yao na kuishauri Serikali kuwa na subra.

Views: 568

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by eddie on November 2, 2013 at 19:11

Ni kweli umoja ni nguvu. Lakini huo umoja unategemea unafanya na nani. Wa spanish wanasema ukijikwaa kwenye jiwe mara mbili ina maana wewe ni mjinga. Wa kenya hawaogopewi ila walioyafanya miaka ile ya 70 inabidi kutoyasahau tutakuwa wajinga tukijikwaa katika jiwe lile lile kwa mara ya pili mfululizo.......!!!

Comment by Zainabu Hamis on November 2, 2013 at 18:20
Twajidanganya wandugu. Umoja ndio kila kitu. Kuwaogopa Wakenya ni udhaifu wa kiakili.
Habari ndio hiyo!
Comment by eddie on November 1, 2013 at 23:05

Ni bora Tanzania ijitoe, umoja huu hautanufaisha Tanzania itanufaisha Mkenya na wengineo......ukiangalia vizuri Kenya hawana cha kutuzidi wao wanatuibia. Huku mitaa ninakoishi, kwa mfano watu wengi wanafikiri mlima kilimanjaro uko Kenya, kwani wao wanatangaza kwenye matangazo ya biashara kama ukitaka kuona kilele cha Africa njoo Kenya.

Na tukikubali kuungana ndio kama tumempa mkenya mlima wote!

Comment by CHA the Optimist on November 1, 2013 at 16:29

Ha ha ha ha ha ha! Jamani, umoja ni nguvu-tu wote Waafrika. Kumbukeni, ndoto za akina Nkrumah, Nyerere na wengineo ilikuwa Afrika kuwa moja, kitu ambacho ni kizuri. Tukiungana, tukawa na dola moja, Rais mmoja, tutakuwa na nguvu na sisi kama walivyo wenzetu. Wenzetu wana nguvu kwa sababu wanaamini katika umoja. Tujifunze jamani.

Nina hamu sana ya kuona siku moja, Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda-zinaongozwa na Rais mmoja. Nina shauku sana ya kuona Arusha ndio inakuwa Washngton ya nchi hizi, nina hamu sana ya kuona tuna pesa iliyo na picha za aidha Kenyatta, au Nyerere zitakazokuwa zinatumika katik nchi hiyo niiotayo itakayoitwa Umoja wa Nchi za Afrika Mashariki (UNA), nina hamu sana ya kuona watu wa nchi hiyo wakizungumza Kiswahili kama lugha yao ya kwanza na English kama lugha yao ya pili. Na baada ya Muungano huo, ningependa siku moja kuona (UNA) inaungana na nchi za kusini mwa Afrika ikiwemo South Afrika, na kuwa na kiongozi mmoja. Na baadaye Afrika yote kuungana na kuwa United States of Africa!  Kelele hizo za hao viongozi wa kidini, na hata hao wanasiasa, ni mufilisi, ni "UOGA" unaotokana na kutokujiamini kutokana na ukweli kwamba hata mitaani katika maisha yetu ya kila siku Watanzania tumekuwa tukiwahofia sana Wakenya hasa kwenye soko la ajira kutokana na uwezo wa hawa ndugu.

Ushauri wangu ni kwamba; tuache uoga na hofu, badala yake tupambane kwa kila namna, ili tuwe aidha sawa na hao tunaowahofia, au hata kuwazidi.

Umoja ni Nguvu, utengano ni Udhaifu. Palipo na wengi vilevile Mungu yupo. How good and how pleasant it would be, before God and man, yea-eah! To see the unification of all Africans, yeah! As it's been said a'ready, let it be done, yeah!  (Bob Marley alituhasa katika wimbo wake Afrika Unite--wimbo ambao kila aliye Mwafrika hana budi kuutukuza)

PamoJah.

Comment by Hashim Said on November 1, 2013 at 9:58

Hakuna sababu kuungana na nchi zenye vita miezi yote ya maisha yao! Tujiondoe!!

Comment by Mama Malaika on November 1, 2013 at 9:38
Kaka Damnan wewe tu twakukatobisha na mkewe. Teh teh teh....
Comment by Mama Malaika on November 1, 2013 at 9:37
Bora wajitoe maana hapa tu tayari matatizo kibao.
Comment by KUNAMBI Jr on November 1, 2013 at 9:32

bora kujitoa tu kwa kweli

Comment by hassan damnan on November 1, 2013 at 7:47

itakuwa si vyema kwa tanzania kujiondowa katika jumuiya ya afrika mashariki hasa ikizigatiwa inchi ya tanzania ni moja kati ya inchi za kiafrika inayopenda ujirani mwema na pia yataka tujuwe tumeshaowana na kuwa ndugu na familia naomba uwamuzi huo uwondolewe jamani umoja ni nguvu shukran

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*