Tulonge

Tazama picha 4 za vifaa imara ambavyo Tulonge alizaliwa akavikuta na hadi sasa vinafanya kazi

Hii ni Redio ambayo Mzee aliinunua Tshs 2000 mwaka 1979, pamoja na mimi kuichezea sana nikiwa mtoto lakini hadi sasa inafanya kazi.

Ni vigumu sana kwa sasa kupata vifaa imara ambavyo hudumu muda mrefu ukilinganisha na miaka ya nyuma. Kwa sasa nipo Dodoma kuwasabahi wazazi, nimeamua kupiga picha baadhi ya vifaa ambavyo nilizaliwa nikavikuta na hadi sasa bado vinafanya kazi vizuri. Vifaa hivi vina zaidi ya miaka 30 toka vinunuliwe. Huwezi vilinganisha na vifaa vya sasa ambavyo haviwezi kudumu kwa muda mrefu.

Hii ni feni ya Sanyo ambayo mzee aliinunua Tshs 600 mwaka 1980. Hadi sasa inafanya kazi bila wasi wasi.

Hii ni pasi ya umeme aina ya Komet ambayo Mzee aliinunua mwaka 1980 Tshs 200. Hadi sasa inapiga mzigo kama kawaida.

Hiki kikombe kilinunuliwa mwaka 1981.

*Jaribu kulinganisha vifaa hivi na vifaa vya siku hizi

Views: 1329

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on March 18, 2013 at 20:17
Mchina kaharibu sana iwe electronics hadi baiskeli.
Comment by Mama Malaika on March 18, 2013 at 20:13
Tulonge umenikusha mbali sana na hiyo radio na kunipa homesick. Mama yangu hadi leo anayo nzima
Comment by Tulonge on March 18, 2013 at 12:58

Hamna noma mzee Eddie

Comment by eddie on March 18, 2013 at 12:47

@Tulonge tunza vizuri hivyo vitu, ughaibuni vitu kama hivyo ni bei mbaya sana hasa kwa wale jamaa wanaofanya collection.

Comment by David Edson Mayanga on March 18, 2013 at 11:55

ebwana eee kweli umesema chamsingi zaidi

Comment by Tulonge on March 18, 2013 at 10:34

Haya Kunambi, wazo lako limefanyiwa kazi

Comment by KUNAMBI Jr on March 18, 2013 at 10:18

Jaman hii ni nzuri sana,mngejitahidi kuweka nembo ya tulonge na kuweka picha moja wapo fb ili watu wajue kama kuna tulonge duniani lol ni wazo tu?

Comment by Dixon Kaishozi on March 18, 2013 at 9:14

Aina hiyo ya Redio hata mimi niliikuta wakati nimezaliwa, sina uhakika kama mzee bado anayo!! Ila nakumbuka wakati tunapiga kanda unabadirisha kwa kutumia hako kwa swichi cha rangi ya chungwa hapo juu.. Good memory!!! teheheee..

Comment by kabegulahamza on March 18, 2013 at 8:29
duh..................!!!!!!!!!!!!!!!
Comment by chaoga on March 17, 2013 at 10:07

made in republic of the people of china...

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*