Tulonge

Uhuru Kenyatta ashinda Urais Kenya

MTOTO wa Rais wa kwanza wa Kenya, Marehemu Rais Jomo Kenyatta, ambaye alikuwa anagombea Urais kwa tiketi ya Chama cha TNA, Uhuru Kenyata ameshinda nafasi hiyo baada ya kumwangusha mpinzani wake Raila Odinga.

Hadi saa 8:35 usiku wa leo Uhuru alikuwa mbele kwa kura 6,173,433 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliyekuwa na kura 5, 340,546 ikiwa ni tofauti ya kura 832,887 na majimbo yaliyo kwisha kutangazwa ni 291/291.

Jumla ya kura zote zilizopigwa na kuhesabiwa kwa nafasi ya Urais ni kura 12,338, 667 kutoka katika majimbo yote ya Uchaguzi 291 huku kura zilizoharibika zikiwa 108975 na kura halali zikibaki 12,222,980.

Katika kinyang’anyiro hicho Wycliffe Musalia Mudavadi anashika nafasi ya tatu akiwa amejikusanyia kura 483,981 nafasi ya nne ikienda kwa Peter Kenneth mwenye kura 72,786.

Mgombea wa Alliance for Real Change,Mohamud Abduba Dida anashika nafasi ya tano akiwa na kura 52,848 akifuatiwa na Mwana mama Martha Karua wa National Rainbow Coalition mwenye kura 43,881 hadi sasa.
Nafasi ya saba katika wagombea hao Urais inakwenda kwa James ole Kiyiapi wa Chama cha Restore and Build Kenya ambaye ana kura 40,998 huku nafasi ya ya nane na mwisho ikishikwa na Paul Kibugi Muite wa chama cha Safina.

Matokeo hayo yatatangazwa rasmi leo saa 5 asubuhi

Hadi kufikia mwisho mambo yalikua hivi:-

Views: 558

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on March 11, 2013 at 9:51

PONGEZI ZAKO UHURU

Comment by Zainabu Hamis on March 10, 2013 at 17:28

tuache unafiki Watanzania na ushabiki usio tija. Tujenge nchi yetu kwanza.

Comment by MGAO SIAMINI,P on March 9, 2013 at 13:25

UHURU KENYATTA anaonekana ana dhamira ya kweli ya kuwavusha wakenya tena ni kiongozi jasiri asieogopa mataifa yenye nguvu kumbuka pamoja na kufikishwa ktk mahakama ya kimataifa lakini bado kasimama hima na wakenya wametuonyesha kwamba wanaweza kujitegemea maana hata baada ya vitisho vya kukosa misaada kwa kuwachagua watu wanao shitakiwa bado wamemchagua shujaa wao.aidha ni fundisho kwa viongozi wa tanzania wanaotegemea kuombaomba.BRAVO wakenya mmeonyesha ukomavu wa demokrasia mungu awabariki mpate utulivu na amani.

Comment by Mjata Daffa on March 9, 2013 at 10:52

Mtoto wa nyoka ni nyoka, wakenya wakubali matokeo na kuanza safari ya kujenga kenya mpya, Raila hana bati japo ni kioongozi mzuri. namshauri UHURU asimuache Odinga kwani nae pia ni mtoto wa nyoka  

Comment by steward kalinga on March 9, 2013 at 10:19

Congrats to Uhuru Kenyata may be you may be the one to save Kenya and Africa as a whole.

This is because in Africa our Leaders have no stands, being driven by western powers, its my dream that one day Africa will have to stand on her self without a support that just kill us instead of helping us

We need leaders who have stands on their decisions, who rule their power and not to be ruled and driven with their interest but for the society

We need leaders who thinks critically what to do for their governments or people an not what to get from the leadership

I will always appreciate M.Gaddafi as one among a strong African leader who has been opposing the rule and dependency from western power, "May God Rest Him in Peace" and that is why he was being killed

AFRICA AFRICA AFRICA, a nice and resourceful continent where all whites desires....lets join together men and women to stand for our continent.... A freedom is not yet

Hongera Kenyata, tunaomba uwaongoze vema wenzetu Wakenya

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*