Tulonge

Ujenzi wa bomba la gesi kuanza leo, Ole wake atakayeligusa

Prof. Sospeter Muhongo

-Ujenzi kuanza leo, Kenya yaomba megawati 1,000

Na Robert Hokororo

SERIKALI imesema haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wananchi, watakaofanya hujuma katika mabomba ya kusafirisha gesi yanayotarajiwa kujengwa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

Sanjari na onyo hilo, pia imewataka Watanzania kuwa na imani na mradi huo, ambao unatarajiwa kuanza leo na kukamilika Desemba mwakani. Imesisitiza kuwa kazi ya ujenzi inakwenda vizuri na kwa usalama mkubwa.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa bomba hilo iliyofanyika katika vituo mbalimbali kuanzia Somanga Fungu mkoani Pwani hadi hifadhi ya mabomba eneo la Mbagala Dar es Salaam.

Profesa Muhongo, alisema kuwa anaridhishwa na ubora wa kazi inayofanywa kwa teknolojia ya juu na kampuni tatu tofauti ambazo zinashirikiana ili kukamilisha mradi huo vizuri na kwa wakati.

Alisema mradi huo utaleta manufaa kwa wananchi wa Tanzania, ambapo mbali na kutoa ajira, pia utaboresha utaalamu wa watalaamu wa Kitanzania kutokana na ajira watakazopata katika kipindi chote utakapokuwa unatekelezwa.

Waziri Muhongo alibainisha kuwa utakapokamlika utaongeza uzalishaji wa megawati 2,015 za nishati ya umeme ifikapo mwaka 2015, ambazo zitafikiwa lengo la kuzalisha megawati 3,000 ambazo ndiyo lengo.

“Ndugu zangu kukamilika kwa bomba hili kutasaidia kuongeza uzalishaji wa umeme hadi kufikia megawati 3,000 mwaka 2015, na tukiweza kufikia hapa tutakuwa na surplus (ziada) ya umeme ambao tutauuza nje ya nchi ili tupate mapato na hili nimekuwa nikilizungumza kila mara,” alisema Prof. Muhongo.

Kuhusu baadhi ya watu kupinga suala la kuuza umeme nje ya nchi, Waziri Muhongo, alisema ili uchumi ukue hatuna budi kuuza umeme na kubainisha kuwa tayari Kenya wameomba kununua megawati 1,000.

Chanzo: jamboconcepts.com/jamboleo/

Views: 257

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*