Tulonge

Utafiti: Dk Slaa aongoza vinara tisa urais 2015

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa

WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo.

 

Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.


Katika matokeo ya utafiti huo uliofanywa Desemba mwaka jana, Dk Slaa anafuatiwa kwa mbali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amefungana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kila mmoja akipata asilimia tisa.

Hata hivyo, licha ya kuongoza, Dk Slaa ameporomoka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kama huo uliofanywa na taasisi hiyo mwaka 2011 ambapo alipata asilimia 42.

Kadhalika, umaarufu wa Pinda ambaye anaongoza miongoni mwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeshuka kwa asilimia tatu kutoka 12 za mwaka juzi, wakati Zitto ameendelea na kiwango kilekile cha asilimia tisa alizopata katika utafiti uliotangulia.

Pia wamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (4) ambaye amefungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (4) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2).

Ikilinganishwa na utafiti wa 2011, Lipumba ameporomoka kwa asilimia tisa.

 

Lowassa amepanda kwa asilimia sita, Dk Magufuli asilimia nne, Mbowe na Membe wamepanda kwa asilimia mbili kila mmoja, wakati Sitta amebaki katika kiwango kilekile cha asilimia mbili.


Hata hivyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi ambao hawana uamuzi wa kuchagua mtu yeyote kati ya hao kwa sasa ni asilimia 18, likiwa ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na utafiti uliotangulia.

CCM yatamba
Katika utafiti huo, CCM kimeonyesha kuwa ni chama ambacho asilimia 52 ya wananchi wangependa kujiunga nacho, kikiwa kimepanda chati kwa asilimia moja kutoka asilimia 51 mwaka jana.

Kwa upande wa Chadema, wananchi ambao wanapenda kujiunga nacho imeshuka kutoka asilimia 35 mwaka 2011 hadi 31 mwaka jana.

Uwezekano mkubwa wa CCM kupanda chati ni kutokana na ukweli kuwa mwaka jana kilikuwa na uchaguzi ulioanzia ngazi ya mashina hadi taifa na kuibua vuguvugu kubwa masikioni mwa wananchi.

Chadema hakikuwa na harakati kubwa za kisiasa ukiacha kampeni ya Movement For Change (M4C), ambayo kwa kiasi haikuwa na pilika kama uchaguzi wa CCM.
Chama kingine ni CUF ambacho kimeporomoka kwa kupata asilimia 10 mwaka 2011 hadi nne mwaka 2012.

Hata hivyo, asilimia ya wananchi kutokutaka kujihusisha na chama chochote imepanda kutoka asilimia mbili mwaka 2011 hadi 12 mwaka 2012.

Rushwa
Katika suala la rushwa nchini, utafiti huo umeonyesha kuwa kati ya watu 10 waliohojiwa, wanne walikuwa na maoni kuwa rushwa imeongezeka kufikia asilimia 41, asilimia 30 walisema iko palepale, asilimia 23 walisema imepungua na asilimia tano hawajui.

 

Utafiti huo unaonyesha kuwa mapambano dhidi ya rushwa hayajabadilika tangu 2011katika taasisi za Serikali ukisema haionekani kama kuna utashi wa kisiasa kupambana na tatizo hilo katika taasisi hizo kama Jeshi la Polisi na Mahakama ambazo zimeonekana kuwa nyuma katika mapambano hayo.


Katika utafiti huo, polisi ndiyo inayoongoza kwa rushwa baada ya asilimia 33 ya watu waliohojiwa kulitaja jeshi hilo, ikifuatiwa na Mahakama asilimia 16 na sekta ya afya ikiwa na asilimia 16.

Utafiti huo umeonyesha matatizo makubwa yanayoikabili nchi kwa sasa ni njaa, gharama za maisha, umaskini, migogoro ya kidini na ukosefu wa ajira.

“Asilimia 50 wametoa maoni kuwa njaa ni tatizo kubwa ikifuatiwa na gharama za maisha asilimia 44, migogoro ya ya kidini asilimia 43 na ukosefu wa ajira asilimia 34.”


“Inamaanisha kuwa rushwa na mfumuko wa bei havichukuliwi kama ni tatizo kwa Watanzania wengi kama ilivyojionyesha mwaka 2011,” inaeleza taarifa ya utafiti huo.

 

Wananchi wameeleza kuwa mambo muhimu ambayo yanatakiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na sekta ya afya kwa asilimia 24, elimu asilimia 21, ajira asilimia 18, chakula asilimia 17 na miundombinu asilimia 16.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz

Views: 1012

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on February 27, 2013 at 4:47
Viongozi roho wamejaa roho mbaya, kutojali wapiga kura, ndio kama hao CCM.
Comment by Mama Malaika on February 27, 2013 at 4:30
Omary... Africa ni tajiri sana kwa natural resources kuanzia madini hadi misitu,. Mfano UK, mito yao mingi kwa bongo tunaita mifereji lakini wazungu unakuta wanasifia na kuitunza kwa juhudi zote. Na maziwa yenyewe madogo na ni manmade. Misitu yao karibu ni ya kupanda na waitunza yalindwa ka macho yote
Comment by Omary on February 27, 2013 at 2:37

Kweli sisi tunajuwa lakutosha mpaka tunalalamika juwa linatuchoma kwani hatuna kazi nalo viongozi wanashindwa kulifanyia kazi unakuta hospital hazina umeme wakina mama wanajifungulia gizani

na hata palipokuwa na umeme tatizo lipo palepale kwani umeme wenyewe haupatikani muda wote

yaani ni shida.com.

huyo mama MUNGU angefanya miujiza akatokea mtu mwenye roho kama ya huyo mama aje atowe uozo ndani ya nchi yetu maana tumechoka kuanzi juu mpoka chini wote wanakwiba mali zetu kila uendapo hakuna unafuu japo  wapo kama Mr Pombe me huwa namkubali sana Mr Pombe hatakama anakula ila kazi yake inaonekana.

Comment by Mama Malaika on February 27, 2013 at 1:32

Sio siri, hata mie hawa majamaa CCM nataka waondoke. Nchi wameirudisha nyuma sana, miaka 52 ya Uhuru nchi inazidi kuwa gizaaaa (umeme), elimu yazidi kutiririka na huduma ya afya ndio usiseme. Ukitoka bungeni tembea dakika chache uingie ndani ya hospital ya mkoa wa Dodoma unakuta wagonjwa hoi mahututi hawajapewa matibabu na wengine wamekata roho eti upungufu wa vifaa huku wabunge wanakamata posho za malaki kwa siku. Utu gani huo jamani???

Comment by Mama Malaika on February 27, 2013 at 1:16

Omary... Bongo anatakiwa mama Angela Merkel wa Germany aje aburuze vigogo hadi ndimi ziwakauke mate. Ha haa haaa... Na kwa utajiri wa maliasili ulioko Tanzania, siajabu hadi amaliza msimu wake mmoja (5yrs) Tanzania itabadirika kuwa kama nchi za west Europe na siajbu 70% ya umeme utakuwa ni wa solar (jua) maana Germany hivi sasa ndio nchi inayoongoza duniani kwa solar technology na matumizi umeme majumbani/viwandani ingawa Germany wakati mwingine jua haliwaki wiki nzima

Comment by Omary on February 27, 2013 at 0:01

Maana  unafika wakati hujui umuamini nani? hata Angela leo tukupe uongozi lazima utake kubomoa kijumba chako ukijenge kisasa zaid hapo unatusahau wapiga kura wako utanunuwa shamba kuubwa kijijini mkwenu utajenga kijijini kujiandaa na kustaafu huku nyuma sisi tunalalamika kuwa umetusahau

haya kuna madeni uliokopa kwa wahindi au misaada uliopata kwa wahindi nao wanataka kurudishiwa fadhira itakubidi ulegeze maadhi ya sheria zako huku sisi tunazidi kuumia umeziba masikio wala hutusikii, hapo ndio hujui nani ni nani? ndipo ninapo changanyikiwa kuwa nani? atakuja kusimama kwaajili yetu? na sio kwaajili yake.

Comment by Omary on February 26, 2013 at 23:43

Me naona angekuja Paul Kagame aongoze kwa msimu 1 tuh. maana hata waha wanaotaka kuongoza sijui watakuwa na lengo moja nasi? au ndio hivyo tena watajifuta machungu na kurudisha pesa zao walizozipoteza?

Comment by ABRAHAM PONERA on February 26, 2013 at 18:21

There you`re, unaonaje uitwe mpiganaji au mwana harakati? Utakapokubali kuitwa hivyo na uwe hivyo kweli kweli,

Comment by ANGELA JULIUS on February 26, 2013 at 17:52

KAKA PONERA NI HII  MPYA INAYOKUJA KWANI UCHAGUZI UJAO TUTAKUWA NA KATIBA MPYA TAYRI NA HIYO NDO ITAKAYOSEMA KWELI, KIUKWELI CCM WANAJIJUA HAWAPENDWI WANALAZIMISHA TUU ROHO ZA WANANCHI KINGUVU NA KUIBA KURA ZETU. NAOMBA SANA AMANI TULIYO NAYO ITAWALE DAIMA NA MILELE ILA TUJARIBU KUFANYA MABADILIKO HASA SISI VIJANA WA SASA.

Comment by ABRAHAM PONERA on February 26, 2013 at 17:22

Sist Angela, kwa mujibu wa Katiba ipi hii tuliyo nayo au tunayoitaraji? Kama ni hii sijui japo kwa kweli hata Mie sijui ni mdudu au kitu au mtu aitwaye chukua chako mapema(ccm) sitaki hata kusikia habari zake. Tattizo la Watanzania si wa kweli Hawafanyi maamuzi sahihi kwenye uchaguzi labda hiyo 2015.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*