Tulonge

Video: Hili ndilo timbwili lililotokea Bungeni Dodoma leo

Leo, Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walitoka nje baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Mhe. Freeman Mbowe kuamriwa atolewe nje na Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai.

Hali hiyo ilitokea wakati wa Majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013.

Mhe. Mbowe alisimama ili achangie lakini aliamriwa na Job Ndugai kukaa chini jambo ambalo hakuliafiki na kuendelea kusimama, jambo lililomsukuma Ndugai kuwaamuru askari wa bunge kumtoa nje Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kitendo kilichozua mzozo.

Mhe. Mbowe aligoma kutolewa nje ya bunge baada ya askari kufika alipokuwa amekaa kwa lengo la kumtoa nje, ndipo mzozo mkubwa ulipotokea ndani ya bunge na kutamatia kwa Wabunge wote wa CHADEMA kutoka nje.

Jana, wakati wa kuchangia muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ukisomwa, wabunge wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi walitoka nje wakishinikiza muswada huo usisomwe hadi maoni ya wadau kutoka Zanzibar yapatikane.

Maelezo na wavuti.com

Views: 620

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by David Edson Mayanga on September 7, 2013 at 1:13

Bado mbona bunge hili iposiku watakuja anzakupiganawao wabunge then tutafuata uraiani .ila sidhani kama mwanamziki faniyako nimuziki leo unakuwa mbunge do haya

Comment by salum kitila on September 6, 2013 at 17:09

Dah hii ni noma kwa hali kama ile...mmh

Comment by Tulonge on September 5, 2013 at 21:51

Daah! hata sielewi nichangie nn. Nimeshindwa kuamini kama hapa ni Bungeni ama sokoni kariakoo

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*