Tulonge

Chuo cha elimu ya biashara, CBE, nchini Tanzania kimeonya kuwa kitawachukulia hatua kali wanafunzi na watumishi wa chuo hicho watakaovaa mavazi yasiyo na staha wala kufuata maadili ya utumishi wa umma.
Kaimu mkuu wa chuo hicho Athumani Ally Ahmed amesema kuwa maamuzi hayo yamo katika sheria mwongozo wa mavazi wa chuo hicho ambapo wanafunzi watakaobainika watachukuliwa hatua kali ikiwemo kuzuiwa kuingia chuoni hapo au kusimamishwa masomo kwa kipindi cha miezi mitatu.
Ahmed alisema wanaume hawatakiwi kuvaa suruali au kaptula "mlegezo" na kuacha sehemu ya makalio nje (Kata K), suruali za kiume zilizopasuliwa, suruali kama zilizochakaa (jeans), kusuka nywele, kuvaa kofia aina ya kapelo, pama au bosholi na kuvaa hereni.
Kwa wanawake mavazi yaliyopigwa marufuku ni nguo fupi (vimini), suruali hasa za jeans zinazobana, kaptula za kike au suruali fupi za kubana (pedopusha), blauzi zinazoacha tumbo, kiuno, kifua na mapaja wazi bila kitu kingine kinachoziba na suruali zinazobana. Vile vile ni marufuku kuvaa sketi fupi zinazoacha wazi mapaja wanapokaa na vazi lolote linaloacha sehemu ya nyuma ya kiuno cha mwanamke wazi au linaloacha wazi sehemu ya juu ya nguo ya ndani wakati amekaa.
Mwanafunzi akiwa shuleni, akakiuka kanuni hizo ataadhibiwa ikiwamo kusimamishwa chuo kwa miezi mitatu.
Adhabu nyingine ni pamoja na kuzuiwa kuingia getini kwa wanaotoka nje ya hosteli na wanaoishi ndani ya eneo la chuo hawatapewa huduma yoyote kama vile kuingia darasani, kantini, maktaba au ofisi yoyote ya chuo.
Ahmed amesema maamuzi hayo magumu yamepitishwa na baraza la utawala la chuo hicho hasa baada ya wanafunzi na watumishi wa chuo hicho kutoheshimu na kukaidi hatua za awali za miongozo ya mavazi ya heshima na yanayoendana na utamaduni wa Kitanzania.

Views: 2551

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Bonielly on May 2, 2012 at 16:41

mama malaika nimeipenda hii picha ya wabotswana, lkn hivi si vinatumika wakati maalumu? na ni mila yao? sasa sisi wa tz hatuna utamaduni wa kibotswana,

Comment by ILYA on April 7, 2012 at 13:38

Mkwe haipendi mwalimu kumvalisha uniform,sio poa hasa kwa mwalimu kumtingisha uniform,atakuwa kama polisi na mwanajeshi.!hahahaha.

Comment by Mama Malaika on April 6, 2012 at 18:30

Hapo umenena kaka Eddie kuhusu uniform, tena itapendeza zaidi iwapo na wao walimu hapo chuoni wangevaa uniform pia. Ha haa haa haa.....

Comment by eddie on April 6, 2012 at 18:07

Dada Mama Malaika nimefurahi sana na maelezo yako......

Mara nyingi huwa nimeongelea uhuru wa mtu kuwa na chaguo lake.Lkini nikaonekana kama vile ni monster hahahaha!

Hapa ume elaborate vizuri sana.

Katika jamii tuko watu wa kila namna, kila mtu anapenda kivyake...si bora kumnyima mtu kuwa na chaguo lake.

Mungu mwenyewe ametuumba hivi tulivyo, huwezi ukamlazimisha mwenzio asifanye/afanye kwa matakwa yake.

Ningeongezea zaidi kwamba hicho chuo kama hakitaki watu wavae vimini basi waanzishe uniform kama zilivyo shule za msingi au secondary, hapo wangemaliza kabisa ubishi!

 

Comment by Mama Malaika on April 5, 2012 at 12:55

Asante sana STEPHEN MINJA kwa uelewa wako. Sehemu yeyote kunapokuwa na cultural imperialism huwezi zuia watu (public) kuvaa nguo watakazo labda iwe kwa sababu za kidini au mtu kazi inamlazimu kama vile army, police, nurse, etc. 

Comment by Stephen Minja on April 5, 2012 at 7:41

Mama Malaika na Christer hongereni mmefunga kazi vimini ni vivazi tu tena vya kileo.Kama mtu hutaki kuviona basi kaa kimya kwani kwa wengine siyo issu ni normal routine ya mavazi. Kuna wasiovaa vimini na bado mambo yao hayasemeki. Swali langu je ni aina gani ya kimini kwa wanawake na Kata K kwa waume chafaa zaidi manake hivyo ni lazina viendelee kuvalika.Mpo walimwengu wa Bongo Land ?

 

Comment by Mama Malaika on April 4, 2012 at 21:00

CHRISTER.... na hiyo zawadi nitafata kweli. Hivyo vimini vya CBE sio vya kutisha, utoto wangu nimeishi Botswana, kule vimini viko sana tu na husikii watu wanapiga kelele. Na wakiamua kuvaa kiasili (tamaduni) ni bora hata ya hivyo vimini. Na wanapenda sana tamaduni zao ukilinganisha na TZ, na ukienda miji midogo au vijiji vilivyo maeneo ya Kalahari Desert kote hadi Namibia nusu uchi ndio asili yao. Nashangaa watu wengine wakiona mwanamke kavaa aonyesha tumbo nje au matiti wanasema eti Africa sio utamaduni wetu, nafikiri hiyo ni kwa east Africa tu ila ukishuka chini ya Malawi hadi ufike kwa wazulu utamaduni wa kuvaa nusu uchi umekuwepo tokea enzi za mababu. Na mika yote hii nimekuwa nikienda nakuta watu hawajabadirika sana...

Comment by Christer on April 4, 2012 at 19:12

Hahahahaahhaaaaa, umenifurahisha sana mama malaika, ukija bongo ntakupa zawadi ya bigijii km huijui muulize Dis kwa kizungu au kiswahili kizuri inaitwaje? kweli kbs km mtu huvai mini au kata k ni wewe na maisha yako binafsi na avaaye pia ni yeye na maisha yake binafsi so long as havunji sheria mi huwa sitaki kuonewa kbs na kwetu nimekua navaa vipensi na mini hizo hizo sasa mtu mwingine akinambia nisivae ntamshangaa ila vimini vya hapo juu ni chiboko kweli kweli @ manka, duuuh mi navaa lakini sio km hivyo, ila pia hao nao waachwe si ndo mavazi walochagua? Waachwe plz!! yaani mi mini ntavaa sana tuuuu mpk labda ntakapochoka mwenyewe ndo ntaacha.

Comment by Mama Malaika on April 3, 2012 at 21:41

CHIRISTER....... Mie iwapo ningekuwa Mwl. hapo CBE na ungekuwa mwanafunzi wangu ingawa mie sivai vimini na vikabutura, ningekuruhusu tu uingie darasani mwangu. Ningechojali sana darasani ni performance yako kimasomo. Nimelelewa kuheshimu uhuru wa mtu kimavazi, lugha, chakula, social norms, personal values and personal beliefs.

Mie niko liberal na watu wengine huwa wanafikiri mie ni atheist. Kwa upande wangu philosophy of life.... to not be limited by fear or narrow definitions, to not build walls around ourselves, but to do our best to find kinship in our inner spirits and understand the deeper truths about our lives. Hivyo kwakuwa sivai vimini haina maana kuwa nitapigia kelele mvaa vimini.

Comment by Christer on April 3, 2012 at 17:12

Tehtheteheteeheteeeee @ Manka, siku moja utaniona usijali. hayo ndo mavazi walochagua kuvaa ss tuwafanyaje? kweli mi navaa vimini ila sio kama vya kwenye picha hapo juu.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*