Tulonge

Viumbe wasioonekana wazidi kuichafua Dunia!

Sayari yetu hii ya dunia baada ya kuumbwa ilikaa miaka mingi mno kabla ya kukaliwa na viumbe wanaoitwa Binadamu.Ambao hapo zamani walitanguliwa na viumbe wengine wajulikanao kama Majini.

Majini ni viumbe walioumbwa kwa moto,miili yao ni miepesi inayowezakupenya sehemu yoyote,tena mwanadamu hana uwezo wa kuiona miili hiyo kwa macho.

Wanao uwezo wa kusafiri masafa marefu kwa muda mfupi,unaoweza kuishangaza akili ya mwanadamu.Kana kwamba wanatumia kasi ya mwanga {nuru},yaani kilometa 300,000 kwa sekunde moja !.

Majini ni viumbe tunaoishi nao duniani,lakini hupenda kujitenga mbali na makazi ya watu,ndio maana huishi misituni,baharini pamoja na majangwani.

Majini hukaa kwa matabaka {koo} na wapo tayari kumshambulia mtu yoyote atakayetaka kuyaharibu makazi yao,na kama yatashindwa vita,basi yatalihama eneo hilo na kwenda kuishi katika eneo lingine.

Mashetani pia ni katika matabaka ya majini,ingawa wao huogopewa sana kutokana na uhusiano wao wa karibu na Ibilisi ambaye ni Baba yao na ndiye huyu anayetusumbua kila siku kwa vishawishi vyake pamoja na kututia wasiwasi ndani ya mioyo yetu.Historia inaonyesha kuwa mashetani ndio waasisi wa uchawi.

Baada ya kifo cha Nabii Suleiman Mwana wa Daud {a.s},mashetani walidai kuwa Nabii Suleiman alikuwa akiwatawala watu kwa kutumia njia za kichawi ndio maana aliwezakuwatawala majini na watu.

Walipata wafuasi wengi mno waliojitokeza kwenda kujifunza uchawi kwa malengo ya kuwadhuru wengine pamoja na kuwatawala.

Rejea Surat Albaqarat Aya 102-103.Ingawa Mwenyeezi Mungu aliwakataza watu kutofuata uzushi wa mashetani dhidi ya Suleiman {a.s} ila watu hawakujali wala kusikia baada ya kunogewa na mafunzo ya kichawi.

Wakaendelea na mafunzo hayo ya uchawi ambayo kwao hayakuwa na faida bali hasara siku hiyo ya malipo.

Cha ajabu ni kwamba inasemekana kuwa hata baadhi ya wasomi na wavumbuzi wa vitu duniani wana uhusiano na mashetani katika kuwasaidia kubuni na kuvumbua vitu vya kisasa,vinavyoweza kumvutia mwanadamu viingiapo Sokoni.

Vitu hivyo ni kama vile: Magari ya bei kubwa,TV,na hata simu za mkononi.Watu hao wenye mahusiano na mashetani hujulikana kama FREEMASONS,na kwa bahati mbaya ndio wanaozidi kulishika soko la dunia kibiashara,wanaenea kwa kasi kote duniani huku wakifanya ufisadi na uharibifu baada ya kuwarubuni watu kwa kuwaahidi utajiri mkubwa iwapo watu hao watakubali kufuata dini ya Shetani !.

Na Chalii_a.k.a_ILYA

Views: 5202

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ILYA on June 10, 2012 at 13:49
VIGOGO  WA FREEMASONS  KATIKA  UKANDA  WA AFRIKA MASHARIKI  NA AFRIKA  KWA UJUMLA
Sir.Andy chande ajitokeza na kusema kuwa yeye ni mmoja wa freemason afrika mashariki .Pia hakuwa nyuma kuwataja viongozi wanaohusika kwenye chama hicho akiwemo rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa .
Pia alimtaja steven kanumba, msanii nguli hapa Tanzania,Baba Riz raisi wa Tz,lowassa,AY,Mr. Blue,na wengineo wengi. Pia hakusita kumtaja yoweri museveni raisi wa uganda,Obama raisi wa marekani,George Bush,Bill Clinton,George washington,Elizabeth malkia wa uingereza na wengineo wengi.
Sir.Andy Chande alitaja yeye kwenye chama hicho ni Grand District Master akiwa amebobea kwa miaka 18 iliyopita.
Alipoulizwa makao yao makuu hapa Tanzania yapo wapi alijibu bila kusita "we are located at sokoine Drive behind kilimanjaro hotel here in Dar es salaam" (tunapatikana barabara ya sokoine nyuma ya hoteli ya kilimanjaro).
Pia Sir. Andy alisema wananyaraka zote za kumiliki jengo hilo toka serikalini. Aliongezea kuwa vikao vyao hufanyika kwa siri nyakati za usiku na mtu akishaingia kwenye chama hiko hatotoka tena
TUKUTANE  KATIKA SEHEMU YA TATU  AMBAPO   TUTAZUNGUMZIA  JUU YA MALENGO YA FREEMASONS NA UJIO WA "NEW WORLD ORDER".......,
ASANTENI
 
Data hizi zimetoka hapa: 
 
Comment by ANGELA JULIUS on June 8, 2012 at 14:45

Nashukuru sana shem kwa maelezo yako @ mama Malaika hivo vitabu sijawahi kuviona kabisa ila i will find time nitafute nisome.

NAKUMBUKA NILIPOKUWA ARUSHA NILIONGEA ISSUE HII YA FREEMASON NA DIXSON, WAPI WEWE DIXSON UELEZE ULIVONIELEZA KABLA SIJAMWAGA MCHELE KWA NJIWA HA HA HA

Comment by ILYA on June 8, 2012 at 0:34

Inasemekana wasanii wa Tanzania nao wameanza kutumia:FREEMASON,dini inayodaiwa kuwa ni dini ya shetani,atakayepata muda anaweza kukandamiza link hii atapa habari murwa:http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/freemason

Comment by ILYA on June 8, 2012 at 0:27

Shem@Hawa wafuasi wana ishara nyingi sana na sielewi kwanini wamezifanya ishara za kuwatambulisha kuwa nyingi,mi nadhani ni ili kuwafanya watu wakabiliane na alama hizo pasina kutambua,maana kama alama unaziona kwa sana tena kibao na tofauti basi huwezi kujiuliza alama hii ina maana ipi na inakusudia nini,maana hutakuwa na muda huo Wa kudadisi mialama kibao iliyozagaa kila sehemu,utaiona ya kawaida tu!,maana alama ziko kibao kila kona unaziona, sasa kuanza kusumbua akili yako na kujadili alama hizi zinahusu nini...... kusema ukweli mtu lazima ujiepusha kuitesa akili yako.Pengine ndio lengo la hawa watu kuwa na alama kibao.Lakini laiti wangelikuwa nazo alam mbili tu,basi nadhani ingelikuwa ni rahisi kuwajua na kuwagundua harakati zao kirahisi.!!hawataki hilo ndio maana wakawa na mialaba ya kuwatambulisha kibao ili kuwapoteza waungwana.!

Lakini kuna alama kubwa kabisa ya kipekee kuliko zote inayowatambulisha Freemasons ,nayo ni hii iitwayoa:

"Square and Compasses".

Katikati ya alama hii kuna herufi "G".

Unaweza kumuuliza Google kw akuandika jina la alama hiyo (Square and Compasses) basi habari zote utazikuta hapo na historia ya alama hiyo na kwa nini katikati kuna alama herufi hiyo "G".

Cha kushangaza sana,viongozi wakubwa wakubwa wa dunia hii leo hii nao ni wafuasi wa dini hii ya FREEMASONS,utawajua tu kupitia alama zao wanazozitumia katika kusalimia wananchi.sehemu hii haitoshi kuonyesha mfano.

Kuhusu alama hiyo ya "Square and Compasses". Hebu tazama pete hiyo nyeusi kwenye mkono wa huyo jamaa hapo kwenye picha ,utaweza kuiona kwa mbali kwenye pete hiyo:

Comment by Mama Malaika on June 7, 2012 at 23:30

ANGELA.... tafuta kitabu kwani kuna vitabu vimeweka siri ya hawa jamaa hadharani hadi hizo nembo zao unazotaka kuzijua majengo yao na kusalimia. Na sio wao tu bali ukisoma vitabu utashangaa kuna organizations nyingine nyingi zinazojiendesha underground kutumia pesa yao kama hawa jamaa kutawala dunia kuanzia USA hadi middle east kwa waarabu ambako wana involved multi billions pounds deals zinazohusisha hadi wafalme nchi za kiarabu. Inatisha sana dunia hii

Comment by Mama Malaika on June 7, 2012 at 20:36

Majaribu ya shetani ni mengi, usikubali kushawishika. Shikiria imani yako siku zote na muombe MUNGU wako wakati wote na yeye atakulinda kiumbe chake

Comment by ANGELA JULIUS on June 7, 2012 at 15:42

ILA NIKIENDA MBELE NIKIRUDI NYUMA INAVOELEKEA IL YA UNAELEWA SANA HII ISSUE NZIMA YA FREEMASON EMBU NIPE HABARI KAMILI EITHER KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE INAWEZA KUTUSAIDIA KUTAMBUA NEMBO ZAO

Comment by ILYA on June 7, 2012 at 13:41

Kaka omary,nikweli kabisa mbinu ya pekee iliyopo ya kuepukana na viumbe hawa wasioonekana a.k.a Mashetani ni kujikurubisha zaidi kwa Mola wako kwa kumtaja sana kwa mujibu wa imani yako,kitendo cha wewe kuwa karibu na Mwenyeezi Munu basi mishetani huwa haipendi,na ikiona hivyo inakukimbia na kukuogopa sana.

Na ndio maana mashetani hutandikwa kwa dua mbali mbali,hapo ndipo utakaposikia kilio cha shetani,anatoa mchozi na kuomba msamaha!,tena anaahidi  kutorudia upumbavu wake!.

Comment by Omary on June 7, 2012 at 10:04

Dah! Kaka uko juu yaani ulioyasema nin ukweli ila siku zote tumtegemee MUNGU hata upitapo sehem halafu ukawa na hofu ya shetan taja jina la MUNGU au soma ujuwavyo kwa imani ulionayo hawatakukaribia tena wakijuwa wewe uko karibu sana na MUNGU watakuogopa

Comment by Lucie on June 7, 2012 at 9:21

Doh, Ss mtu atagunduaje hizo bidhaa zao?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*