Tulonge

Wachangia kondomu, wengine watumia mifuko ya plastiki kujamiiana

Baadhi ya wananchi mkoani Kilimanjaro wamelazimika kutumia mifuko ya plastiki (marlboro) kujikinga na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI huku wengine wakichangia kondomu, jambo ambalo ni hatari na linaelezewa kuwa moja ya chanzo cha ongezeko la maambukizo mapya ya ugonjwa huo mkoani humo.

Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizo ya ugonjwa wa Ukimwikatika Mkoa wa Kilimanjaro, kimepanda kutoka asilimia 1.9 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 3.8 mwaka 2011/2012.

Akizungumza na gazeti la MAJIRA ofisini kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali, linalojihusisha na mapambano dhidi ya UKIMWI mkoani Kilimanjaro (KACA) Faraji Swai alisema wananchi wa maeneo ya vijijini wako hatarini zaidi kupata maambukizo ya ugonjwa ya ukimwikutokana na kwamba wengi bado hawajafikiwa.

Alisema Shirika la Kacakatika utoaji elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI kwa jamii, wamefika katika baadhi ya vijiji mkoani Kilimanjaro na kuwakuta wananchi wakitumia mifuko ya plastiki (malboro) kama kinga ya kujikinga na maambukizo ya UKIMWI huku wengine wakichangia kondomu jambo ambalo liliwashangaza.

Alisema vijiji ambavyo walikuta wananchi wakitumia malboro kujikinga na Ukimwina kuchangia kondomu ni
 
pamoja na Kahe, Mikocheni, Newland na TPC vyote vya Wilaya ya Moshi, huku baadhi ya mitaa katika Kata ya Njoro Manispaa ya Moshi wakikutwa nao wakichangia kondomu moja zaidi ya mtu mmoja.

"Ni jambo la kushangaza kwani yapo maeneo katika Mkoa huu wa Kilimanjaro ambayo tumefika kutoa elimu ya kujikinga na maambukizo ya UKIMWI na wananchi kutueleza kuwa wao hutumia malboro kama kondomu kujikinga na ugonjwa huo huku wengine wakifua kondomu mara baada ya kutumia ili kutumia tena wakati mwingine au kumpa mwenzake naye ajikinge, kwa kweli hii ni hatari sana," alisema Swai.

Alisema maeneo ya mjini kondomu zimekuwa zikizagaa kwa kukosa watumiaji lakini yapo maeneo ya vijijini yenye uhitaji mkubwa na hayajafikiwa jambo ambalo limesababisha kasi ya ukimwikatika maeneo hayo kuzidi kukua.

Alisema maeneo mengine ambayo yameonekana kuwa na kasi ya maambukizo ya UKIMWI na yanauhitaji mkubwa wa kondomu ni Kibosho, Mwika na Marangu Mtoni hivyo kunahitajika jitihada za makusudi za kuwanusuru wananchi wa maeneo hayo.

Swai aliongeza kuwa zipo sababu nyingi ambazo zinachangia kasi ya maambukizo mapya ya Ukimwiambapo ni pamoja na umaskini wa kupindukia ambao huwafanya wasichana wengi hususan wa vyuo vikuu kujiingiza kwenye biashara ya kuuza miili.

Alisema sababu nyingine ni baadhi ya watu ambao wameshajitambua kupata maambukizo ya Ukimwikuueneza kwa makusudi, ulevi wa kupindukia, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na vijana wengi kutokuwa na kazi za kufanya na hivyo kujiingiza kwenye biashara za ngono.

"Kwa sasa wananchi wengi hawaogopi tena UKIMWI, wanaona ni hali ya kawaida lakini sisi kama shirika tumekuwa tukijitahidi kutoa elimu hasa kwa vijana kwani kama hatutakuwa makini tutaipoteza nguvu kazi ya taifa hapo baadaye," alisema.

"Sheria ya UKIMWI inasema mtu ambaye atabainika kuambukiza ugonjwa huo kwa makusudi ashtakiwe, sasa tunaomba ifanye kazi na Serikali iweke mkazo katika hili, ihakikishe wale wote watakaobainika kukiuka sheria hii wanachukuliwa hatua kali za kisheria," alisema.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, akizungumzia ongezeko la maambukizo ya ugonjwa wa UKIMWI kwa mkoa huo, alisema imeonekana kupanda mara dufu, hivyo kuwataka wananchi mkoani humo kubadili tabia na kuepuka ngono zembe.
Florah Temba, MAJIRA, Moshi

Views: 402

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Swedi on August 21, 2013 at 12:05

Sasa na hiyo mifuko ya malboro inapigwa marufuku ina maana watabakia na zile za kufua na kuanika na kuazimana peke yake... mamamamamamaaweeeeeeeeeeeeeeeeee

Comment by Mama Malaika on August 15, 2013 at 18:45
Hii yote ni poverty, ignorance au ndio tabia yetu ya kuendekeza ngono leo huyu kesho yule??
Comment by Omar on August 15, 2013 at 13:54
Ukimwi ishakuwa ni biashara kama nyengine tu sasa ukiisha nyinyi mulioanzisha mradi wa kuutokomeza mtakula wapi.ukimwi hauzuiliki hata kwa condom za bati dawa ni kuacha tu uasherati.ukimwi ni sawa na anti virus tu kwenye computer.lakini hilo lijulikane ukimwi ni moja ya biashara za watu walizobuni waingize hewa. Hii ndiyo 21 century.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*