Tulonge

Wachezaji wanne wa Yanga wadaiwa kuuza mechi

Kipa wa Yanga Juka Kasseja wakiwa amedua baada ya Hamis Tambwe kufunga bao la pili kwa njia ya penalti

Siku moja baada ya Klabu ya Simba kuibuka kidedea katika mechi ya nani mtani jembe,kufuatia kichapo cha aibu cha mabao 3-1 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,Wazee wa klabu ya Yanga wanadaiwa kutafuta mchawi, hata hivyo taarifa za ndani zinadai kwamba mlinda mlango wa timu hiyo Juma Kasseja ndiyo mtu wa kwanza kutupiwa lawama hizo.

Mabao 2 yaliyofungwa na msambuliaji wa Kimataifa kutoka Burundi Hamis Tambwe na 1 la Hawadhi Juma yamemfanya Kasseja kuwa katika lawama kubwa huku ikidaiwa kwamba alisajiliwa kibiashara zaidi lakini si kwa malengo ya kuisadia timu hasa katika mechi za watani wajadi na kwamba ana mapenzi na Simba.

"Sisi tangu mwanzo tulikuwa na mashaka na usajiri wa Kasseja kuhusu kiwango chake, lakini pili tunafahamu fika kwamba Kasseja ni shabiki mwenye kadi ya Simba tatu Kasseja anapenda pesa ukimtengea pesa ni lazima aisaliti timu yake, hivyo tulikuwa na wasiwasi sana katika suala hili lakini tukasema ngoja tuone mwisho wao kwani siku hivi Yanga ina viongozi wasiopenda kushauriwa na hawana uchungu na timu bali wanafanya biashara,"alisema kiongozi mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe mtandaoni.

Kocha Mkuu wa Simba Zdravko Logarusic, akiruka juu baada ya timu yake kupata bao la kwanza dhidi ya Yanga.Picha zote na Habarimpya.com

Yanga ambayo ilikuwa na kikosi chake chote katika mechi hiyo, ilipata bao la kufutia machozi iliyofungwa kwa kichwa na mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka Uganda Emmanuel Okwi aliyeingia kipindi cha pili kuchukuwa nafasi ya Didie Kavumbagu.

Mbali na Kasseja wachesaji wengine wanaodaiwa kuvuta kitita katika mechi hiyo ni pamoja na Nahodha Nadir Haroub 'Canavaro' ,Kelvin Yonda na Athuman Iddi "Chuji' kwa madai kwamba hawakuipa mechi hiyo umuhimu kwa kuwa haikuwa mechi ya ligi, "Sikiliza bwana mwandishi ni kwambie kitu mechi hii imeuzwa, kwani wenzetu walitumia nguvu kubwa kuwanunua wachezaji ili walinde heshma yao, baada ya Yanga kufanikiwa kunyakuwa kitita kikubwa cha shindano la nani mtani jembe na wachezaji niliowataja hapo juu ndiyo waliopokea mlungura huo, alisema kiongozi mwingine wa timu hiyo.

Views: 524

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mjata Daffa on December 23, 2013 at 8:17

wachani manenoneno tujipange

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*