Tulonge

Waganga wa siku hizi wapo wazi kabisa

Hili ni bango linalomnadi mganga mwenye uwezo wa kumpatia mtu hela za majini lililopo eneo la Sinza Mori. Siku za nyuma ilikuwa ni vigumu sana kukutana na mabango ya aina hii. Mambo ya kutafuta hela za majini ilikua ni siri. Ila kwa sasa ni wazi wazi

Views: 1976

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Jeath Justin Prosper on April 11, 2014 at 13:41

nahisi pia ni kwa saababu wanalipia maangazo kwa jiji....sidhani kama wanabandika bure. Watakua wanalipia kwa serikali za mitaa. 

Comment by Jeath Justin Prosper on April 11, 2014 at 13:40

Biashara ni Matangazo!

Comment by Mama Malaika on March 5, 2014 at 19:26
Tulonge una matata sana wewe. Ha haaa haaaa...

Hii kasumba ya kuacha watu wafanye matangazo na biashara zao kiholela ndi yaleta matatizo, jiji limekuwa hovyo. Muda si mrefu wataweka mabango hadi nguzo/miti makaburini au maeneo ya makaburi
Comment by CHA the Optimist on February 19, 2014 at 14:07

Inaonesha kuna tatizo kubwa sana la nguvu za kiume hasa mijini. Matangazo kama haya mikoani hayapo kabisa.

 

Mama M--Tanzania kila kitu ni shaghalabagala. Wajua baba au mama wa nyumba akiwa shaghalabagala, hata watoto nao watakuwa hivyohivyo

Comment by Tulonge on February 18, 2014 at 20:46

-Hahahhahhahahaaa Mjata umenivunja mbavu na comments zako. Tatizo unaweza ukatumia hiyo dawa halafu 'abdala kichwa wazi' akanenepa kupita kiasi.Unashangaa anakua kama mtwangio. Naona shemeji alistuka, usije ukamuua bure.

-Mama Malaika hao hawalipi cha kodi wala nn, wengi wao wanabandika kwenye nguzo za umeme

Comment by Mjata Daffa on February 18, 2014 at 11:18

asante sana dada yangu bahati nzuri nilikuwa na WIFE  kama kawaida yetu ikabidi nimtanie nikamwambie nakwenda kununu ile dawa alicheka baadae akakichukua kile kikaratasi na kukichana. sijui alizani nitaenda kweli hahahahahaha. woga wake tu hata asinge chana nisingeenda kufanya upumbavu huo kwanza M/Mungu amenijaalia sihitaji nyongeza wala pungufu.

Comment by Mama Malaika on February 18, 2014 at 10:30
Duh! Pole Mjata Daffa. Hiyo si busara na pia ni kero ukizingatia mtu una drive na mwingine ana ku- distract, hata humo kwa office unajikuta washindwa ku-concentrate kwa kufikiria hicho kikaratasi.

Kusema kweli haya mabango sirikali ifanye utaratibu kuyapunguza kwa kutoza kodi hayo mabango ili kuyapunguza. Hasa mji wa Dar ile unaingia tu wakumbana nayo ya kila ujumbe kuanzia vyama vya siasa hadi waganga wa kienyeji
Comment by Mjata Daffa on February 18, 2014 at 8:49

Nchi hii sasa imegeuzwa shamba la bibi, hata wewe ukiwa na chochote unaweza kubandika popote na hutaulizwa na yeyete.

mfano leo nikiwa naendesha gari kuelekea ofisini alipita kijana dirishani akanitumbukizia kikaratasi cha tangazo linlosema Njoo upate dawa ya kurefusha na kunene pesha uume, asume ningekuwa na mkwe wangu ndani ya gari ningeweka wapi uso wangu? hii sijaipenda 

Comment by Mama Malaika on February 18, 2014 at 2:21
Na kweli watozwe na kodi. Ila napenda kujua hayo mabango wanalipia au??
Comment by paul michael on February 18, 2014 at 0:37

ifikie mahali wawe wanatoa kodi sasa

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*