Tulonge

Wakati mwingine kifo huwa kimetulia zake ila kuna watu wanaki-beep, hebu angalia hii bembea (picha 4)

Sina hakika na utimamu wa akili ya mtu aliyefunga hii bembea hapa. Ukisikia kuki-beep kifo ndo huku, sasa ngoja kiwapigie sijui watapokea au vipi.

Views: 831

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Jeath Justin Prosper on July 12, 2013 at 15:01

Hii ndo adventure ya ukweli.............killing up the big funs for fans....

Comment by Mama Malaika on July 11, 2013 at 19:01
Bembea hii nchi za Ulaya ni kawaida, hata mwananagu na baba yake wanabembea hapo bila uoga. Ukizaliwa west hasa mtoto wa kiume michezo hii ni kawaida sana kwani tokea utoto unakuwa exposed kwenye michezo ya hatari na pia lifestyle sio kubanwa ndio maana wanakuwa na free spirit. Wakuta vitoto vidogo vya kizungu umri miaka 4 vinapanda miti mirefu na kukwea kwenye mabembea tena wakiwa na wazazi wao wanawatizama wala hawakatazwi. Tanzania mtoto akipanda mti mfupi tu wa mpera anatiwa bakora kisawasawa, haya niambie hiyo free spirit ita developed vipi kwa mtoto hadi aje apate ujasiri huu??
Comment by KUNAMBI Jr on July 11, 2013 at 16:48

HAHA haha haha we Dis kweli bangi,lkn ujue wazungu bhana wana akili mpk zimewazidi wanapenda kufanya mambo ya ajabu ajabu sana

Comment by ANGELA JULIUS on July 11, 2013 at 16:41

ukiangalia hizo bembea kwa umakini utaona kuwa wala hawaipandii juu ndo wakalie hicho kitako ikitulia ikakaa sawa utaona anapandia chini bembea ikishachanganya lazima upae mbali na hapo kinachotisha ni hiyo mandhali ya eneo kunaonekana ni milima na mabonde na huko juu  ni sehemu waliposet hiyo bembea ni picha tuu ndo inatisha lkn nina uhakika wameanzia chini.

Comment by BARAKA FRANCO CHIBIRITI on July 11, 2013 at 15:03

Unajua Mkuu Tulonge, Wazungu sio waoga kabisa kwa mambo ya hatari kama haya....hawaogopi kufa kabisa. Yaani ukiona vitu vya hatari wanavyofanya mpaka utashangaa kabisa na kuogopa sana. Yaani mimi huwa naangalia mpaka nasema basi, hasa michezo ambayo huwa wanafanya ya ajabu ajabu tu....mpaka unashindwa kuelewa. Lakini wao ndo walivyo, hawana shida kabisa kwa mambo ya hatari....hawaogopi kabisa. Angalia sasa kama hapa ilivyo hatari...lakini wao kama mchezo tu! Na huwa wakati mwingine kweli wanakufa kabisa, ndipo wanaacha ....lakini vinginevyo hawaachi.

Comment by MGAO SIAMINI,P on July 11, 2013 at 13:36

hawa jamaa sio waoga

Comment by Monica on July 11, 2013 at 12:20
Kila nafsi itaonja Mauti,.kufa ni kufa mbaya kutangulia,.hata Kwa fimbo au ahadi ya mamilioni bado sijabembea,.Anjela Hiyo bembea unaipandia kwenye mti wenye ngazi kwani ukisimama chini huwez kuipanda,.neno kilema halichezi mbali na wewe,.Dismas umeitoa nchi gani hiyo?nina uhakika sio TZ,.heeeheeee
Comment by Tulonge on July 11, 2013 at 7:36

Unafanya mchezo ww Angela, hapo huwezi nishawishi hata kwa dawa.Kifo nje nje hapo

Comment by ANANGISYE KEFA on July 11, 2013 at 7:35

hii inanikumbusha jamaa mmoja alikuwa anafanya ule mchezo wa kuruka kwenye mabonde marefu huku ukiwa umejifunga kamba mguuni na hii ilitokea kwenye maporomoko ya Victoria ya mto Zambezi akiwa hewani si ile kamba ikakatika lakini bahati nzuri wa okoaji wakamuwahi akaokolewa kwa hiyo hizo kamba siyo za kuziamini kabisa.

Comment by ANGELA JULIUS on July 11, 2013 at 6:51

Tulonge hizo bembea wala si hatari vile unavofikilia wewe umeona picha zilizopigwa kwa mbali ndo mana umetishika na hata kama ikitokea imekatika kufa hafi ila maumivu atakayoyapata mwaka mzima hoi bin taaban lkn pia ukicheki hizo kamba ni imara na zimefungwa kwa ustadi wa hali juu halafu wenzetu unaweza kukuta wamezikatia na bima ha ha ha

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*