Tulonge

Walimu waelezea uhusiano wa Kamanda Barlow na Dorothy (mwanamke aliyekua nae kwenye gari)

Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Nyamagana wamevunja ukimya na kueleza kile kinachodaiwa ni mahusiano kati ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow, na mwalimu mwenzao, Dorothy Moses.

Wakizungumza na NIPASHE shuleni hapo jana, pia walielezea kusikitishwa kwao na jinsi tukio hilo la mauaji ya RPC lilivyotokea mbele ya mwalimu mwenzao, Dorothy Moses aliyeuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Jumamosi eneo la Kitangiri, jijini Mwanza.

Mwalimu Dorothy ndiye aliyekuwa na RPC Barlow ndani ya gari wakati watu wanaosadikiwa kuwa majambazi walipowavamia na kumuua kwa kumpiga risasi Kamanda huyo.

Katika mahojiano hayo Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Mary Ngalula, alisema wanamuonea huruma mwalimu mwenzao kutokana na kushuhudia tukio hilo la kutisha.

Alisema wanamsikitikia kwa sababu jamii imeanza kumfikiria vibaya kwa kudhani anahusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji hayo.

“Tunamuonea huruma mwalimu mwenzetu kutokana na maneno tunayoyasikia, lakini sisi tuko pamoja naye kwa sababu tunamfahamu ni mtu safi, na hivi tunajiandaa kwenda kumuona na kumtia moyo ili amudu kuilea familia yake kwani ni mjane,” alisema.

Mwalimu Baraka Magafu alisema tofauti na hisia za baadhi ya watu kuhusu uhusiano wa Mwalimu Dorothy na Kamanda Barlow, wao (walimu) wanafahamu kuwa ni watu wa kabila moja wanaotoka kijiji kimoja huko Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Alibainisha kuwa Mwalimu Dorothy amekuwa ni mtu anayejihusisha sana na shughuli mbalimbali za watu wa kabila lake (Wachagga), hivyo hakuna sababu ya kumfikiria vibaya kwa sababu tu mtu aliyekuwa amemsindikiza nyumbani wakitokea kwenye kikao cha maandalizi ya harusi aliuawa kwa kupigwa risasi.

“Ukifuatilia mwenendo wa tukio lote, utaona kwamba kilichotokea ni bahati mbaya na kingeweza kumtokea yeyote, kwani Barlow alikuwa akimsindikiza Mwalimu Dorothy nyumbani kwake, na hata baada ya tukio, alipowapigia simu wenzao waliokuwa nao kwenye kikao walikuwa ndipo na wao wanafika majumbani mwao,” alisema.

Aliongeza kwamba katika mazingira kama hayo ni makosa kuwa na mtazamo hasi dhidi ya Mwalimu Dorothy kama ambavyo baadhi ya watu wameanza kuvumisha kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Ni sehemu katika habari iliyopo kwenye gazeti la NIPASHE

Views: 561

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on October 17, 2012 at 11:51

UONGO NA UKWELI HUWA NI KAMA MAJI NA MAFUTA, HIVYO UKWELI UTAJULIKANA TU, POLE MAMA.

Comment by Mercy Kimario on October 17, 2012 at 8:49

Pole mwalimu Dorothy, whatever the case might be, we songa mbele kuzushiwa kupo na wazushaji ni watu.  Vidole vya watu visikuharibie malengo yako.

Comment by Regina Lipyana Haule on October 17, 2012 at 8:40

ila watu wasichukulie hilo swala kwakua alikuwa na huyu mjane yawezekana kuna sababu nyengine huyo mjane amefanywa kama kupandikiziwa kwa kuwa kifo amekishuhudia

Comment by Mama Malaika on October 16, 2012 at 16:24

Sasa hao majambazi yamemuua tu huyo bwana bila kuchukua mali yeyote? Au walikuwa sio majambazi bali walikwenda na nia nyingine?

Comment by Dixon Kaishozi on October 16, 2012 at 15:38

Pole pole ukweli utajulikana!! Kama kweli huyo mwalimu alikuwa na mahusiano na huyo kamanda Basi alikuwa anafanya makosa makubwa sana kwa Mungu wake, Familia yake, Familia ya marehemu na kwa jamii kwa ujumla! Kwani yeye kuwa mjane haimaanishi awe na mahusiano na mtu mwenye familia nyingine tayari..

Na kama si kweli kama tunavyo yasikia Basi nampa pole sana na amtegemee Mungu atayashinda yote!

Comment by Tulonge on October 16, 2012 at 15:10

Kumbe huyo mwanamama ni mjane. Nampa pole sana.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*