Tulonge

Wamachinga: Ujio wa Rais Obama umetuletea njaa

Dar es Salaam. Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara katikati ya jiji na kuondolewa kutokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama, wamelalamika kuwa sasa wanakabiliwa na maisha magumu.

Obama anatarajia kuwasili nchini kesho katika ziara ya kikazi ya siku mbili huku akiambatana na ujumbe wa watu wapatao 700.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili, wafanyabishara hao walisema kuondolewa huko kumewafanya kukosa kipato walichokuwa wakikipata hivyo kusababisha ugumu wa maisha.

Frank Mkama alilalamika: “Hapa Serikali isiseme kuwa wanafanya usafi wa jiji kwa kuwaondoa wafanyabiashara hii si kweli! Mbona hawakufanya zamani, hapa ni Obama ndiyo amesababisha sisi tukaondolewa.”

“Hivi sasa maisha yangu yamekuwa magumu. Kipato ambacho nilikuwa nakipata hapa na kula na familia yangu sasa sikipati.”

Naye, Elizabeth Makata alilalamika Serikali ilipaswa kuwaandaa wananchi kwa kuwaeleza ujio huo wa Obama watanufaika vipi na si kuwafanya waathirike kwa kuvunjiwa maeneo yao.

Alielezea wasiwasi kuwa huenda baada ya ziara hiyo wakashindwa kuendelea na biashara kwa kuwa watakuwa wamekula mitaji.

Kwa upande wake, Ramadhan Issa alisema ziara hiyo ya Rais Obama imeathri maisha yake kutokana na kuvunjiwa kibanda alichokuwa akifanyia biashara hivyo hajui hatima ya maisha yake.

Kadhalika Mwananchi Jumapili iliwashuhudia askari polisi wakionekana kuongezeka katikati ya jiji wakipita huko na kule kuhakikisha hali ya usalama inaimarika.

Pia hali ya usafi imeendelea kuimarika kutokana na ujio kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa kwa lengo la kusafisha mazingira.

Licha kwamba wafanyabiashara hao wameondolewa hivi karibuni baadhi yao wameanza kurejea kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Chanzo:mwananchi.co.tz

Views: 549

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on July 4, 2013 at 3:02
Huo ni utamaduni wa Tanzania na Africa kutangazwa na sio nchi zote duniani wafanya hivyo kwani wana taratibu zao na mambo mengi. Kikwete mara nyingi kaingia UK tunafanya kusikia kwenye blogs za watanzania na radio BBC idhaa ya Kiswahili na sio BBC channel ya wao waingereza au Sky, ITV, etc.

Wamachinga hawajaanza last year kuuza vitu vyao barabarani. Sirikali ilipaswa kuwepo taratibu na kuitekeleza tokea miaka ya 90 mwanzoni wamachinga walipokuwa wachache kuondolewa barabarani sio sasa eti kusikia ugeni ndio wanafukuzwa. Obama aondokapo machinga wanarudi barabarani na siku nyingine akija raisi wa G8 watafukuzwa tena, hiyo si haki.
Infrastructure kuwa mbaya TZ inasababishwa na plan mbaya zinazoandaliwa na hao decision makers tena ki-ujanja ujanja na ufisi. Mfano TZ ku-phased out analogue TV to digital, hakukuwa na umuhimu kabisa. Waingereza na ujanja wao wote hadi sasa kuna sehemu UK zatumia analogue TV, na hata simu mkononi baadhi ya sehemu vijijini baadhi ya mobile phone networks shida hazishiki. Sio kwamba wako nyuma bali hicho kidogo walicho nacho (pesa) kinaelekezwa kwenye basic needs kama vile manunuzi ya vifaa na madawa ya hospitals, kukarabati na kupanua barabara (flyovers) kupunguza foleni kwenye makutano barabara, kugharamia maji safi/salama na maji chafu ili kulinda afya ya wananchi, n.k.
Comment by MGAO SIAMINI,P on July 3, 2013 at 22:10

@JEMEDALI ck zote ni lazima tujifunze kwa waliofanikiwa, ujio wa mgeni nyumbani ni lazima uwe furaha kwa familia. ukiona mgeni amekuja nyumbani halafu watoto mnakatazwa hata kuangalia tv mpaka ondoke bila shaka uhuru umebanwa na baba maana mgeni hawezi kujipangia na huo ni utumwa wa mawazo. SEMA TU 'UMASIKINI HULETA WOGA'

Comment by jemadari mimi on July 3, 2013 at 8:32

Unajua ni lzm tuseme ukweli hata kama wengine watachukia,binafsi siwezi kumlaumu rais ama media kutangaza ujio wa obama au viongozi wengine wa nchi mbalimbali wanaokuja hapa nchini.media zote duniani zipo kwa kusudio la kutoa habari kwa wananchi ili kujua nini kinaendelea ktk hii dunia,sasa unaposema wasitangaze angie kimyakimya ni kinyume na tamaduni za kitanzania.

Jamani ni kweli watu wameathirika ktk mihangahiko yao ya kupata riziki,lkn unapomlaumu rais eti yeye ni ndio tatizo unakosea kabisa ,wanachi wengi wanafanya biashara zao ktk barabara kuu ambako ndiko kunakopita misafara ya marais,je kwa mazingra ya bongo ulitaka vijana wale wanauuza maji,pipi,vitu mbalimbali waachwe tu barabarani.Hivi kuna barabara ipi inaweza kutumika kupitisha misafara ya marais bila kuingilia shughuli za wananchi kwa hapa bongo.

Tatizo la wabongo wengi wanataka kufananisha marekani na tanzania wakati wale wametuzidi kwa kila jambo wana miundombinu bora kabisa tofauti na sisi.

Comment by Mama Malaika on July 1, 2013 at 21:36
Halima Omary... Raisi wako akipita New York City or Washington DC msafara wake ni magari sio zaidi ya 2 tena hakuna hata mtu barabarani anayejua kuwa raisi wa TZ kaingia, barabara magari kama kawaida. Na wala hutosikia mainstream media zikitangaza ujio, wanaingia kimya kimya na kutoka kimya kimya.
Comment by Mama Malaika on July 1, 2013 at 21:29
We must emancipate ourselves from mental slavery. Obama ingawa ana ngozi nyeusi bado ana moral values za kaskazini magharibi mwa dunia wasikotetemekea/sujudu watu. Huu ni upuuzi wa raisi wa TZ, hata New York City & London zina wachuuzi kama machinga walioko Dar es salaam, tena ukumbi wa bunge la Uingereza kuna homeless wanapiga kambi (tents) pale mbele viongozi wa dunia wanapopita kuingia bungeni au kuelekea kwa Waziri mkuu (no. 10 Downing Street). Hata siku moja wachuuzi au homeless wa Washington DC or New York City hawezi timuliwa na blankets//boxes zake eti Obama anapita au afanya jogging. Au New York City hutosikia wanatimuliwa eti viongozi wa dunia wanapita kuhudhuria mkutano wa Umoja wa mataifa.
Comment by halima omary on July 1, 2013 at 18:41

ivi kweli haya yanayofanywa ni sahihi? na rais wetu atafanyiwa mambo hayo akienda huko?  tutakua dhalili mpaka lini?

Comment by Christer on July 1, 2013 at 9:47

Hii nchi jamani, ptuuuuuuuuuuuuuu

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*