Tulonge

Waziri Mkuu aunda Tume uchunguzi kufuatia matokea mabaya ya kidato cha nne 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.

Wadau wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).

Amesema Serikali inawaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.

Views: 640

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by emanuel Lyanga L. on February 25, 2013 at 19:38

TUME HAISAIDII KWANI KUNA MTANZANIA ASIYEJUA MATATIZO YA SHULE ZA KATA. SASA KWA NINI TUPOTEZE PESA KWA MAJIBU YANAYOJULIKANA.

Comment by Mama Malaika on February 25, 2013 at 12:37

Wazazi/walezi nchi nzima washikamane na kudai haki ya watoto wao hadi kieleweke. Hawa viongozi wote wamesoma bure na bado watoto wao wanasoma kulipiwa school fees kwa pesa za walala hoi, na bado wanageuza matokeo mabaya mtaji wa kujipatia pesa/malupulu kupitia tume inayoundwa.

Comment by Dixon Kaishozi on February 25, 2013 at 12:34

Tehehee.. Jichekee tu @ Christer maana stress ni nyingi na hakuna jipya hapa!!

Comment by Christer on February 25, 2013 at 12:18

Haahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa Dixon, unanivunja mbavu mie

Comment by Dixon Kaishozi on February 25, 2013 at 12:13

Kidumu chama chetu... kidumuuuuuuu... Zidumu sera zetu .... Zidumuuuuuuuu... Zidumu TUME tunazounda.. Zidumuuuuuuuuuu Na hi tume iliyoundwa idumu .. Idumuuuuuu...

Tulianza, tukaweza, tumeweza na Tunasonga mbele..

Comment by Christer on February 25, 2013 at 9:11

Haahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa TUMIEN @ Lyehagi

Comment by Lyehagi Mazuli Mhuli Jr. on February 24, 2013 at 20:22

This is just bribing people as the matter seems to be a burning issue to moment! For sure nothing will be implemented from the TUME as it is known as TUMIENI

Comment by Lyehagi Mazuli Mhuli Jr. on February 24, 2013 at 20:18

Hii ndo kawaida ya Serikali yetu, tume bila implementation,  kazi kubwa ni kumaliza fedha za walipa kodi tu.

Swali: Ni lini tume ilifanya kazi yake na matokeo yakatangazwa na kufanyiwa kazi?

          Lini ambapo elimu ya Tanzania ilifanyiwa utafiti?

          Je, wanafunzi kufeli wameanza leo? au ndo leo wameliona hili?

Kwa nini serikali isikimbilie mahakamani kuzuia baraza kufelisha wanafunzi hivi kama ilivyokimbilia mahakamani wakati wa mgomo wa walimu?

Sababu zote zinajulikana sana ila ni UZANDIKI, WIZI, UNAFIKI WA KISIASA tu, Hakuna jipya..

Comment by Mama Malaika on February 24, 2013 at 18:11
Halafu huyu bwana anikera sana sio siri! Wizi wa mchana kweupe, tume gani wakati sababu zote za matokeo mabaya ziko wazi?
Comment by Tulonge on February 24, 2013 at 10:13

Utaona kama wataiweka sababu ya Walimu kukosa haki zao za msingi kama moja ya sababu ya wanafunzi kufeli. Watataja sababu nyingine nyingine tu.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*