Tulonge

Waziri Mkuu aunda Tume uchunguzi kufuatia matokea mabaya ya kidato cha nne 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.

Wadau wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).

Amesema Serikali inawaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.

Views: 638

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on February 23, 2013 at 22:27

Hiyo danganya toto kuizima hoja,tume ambazo zingeleta tija labda zile za mbatia alizo lishauri bunge halafu wabunge matahira wa chama cha mapinduzi wakapinga kwa nguvu zote kisa mahaba ya chama chao.mi nawambia imekula kwao 2015 hawaruki

Comment by Wa Kimberly on February 23, 2013 at 21:37

Tume zinaundwa kila siku ila hawarudigi hata siku moja kutuambia matokeo ya hizo tume.

Wanakula pesa za wananchi tuu hao.

Comment by ABRAHAM PONERA on February 23, 2013 at 20:32

Hapo ni kutengenezeana ulaji, lakini wacha tuone wataimbuka na jipya gani? Ila watakayoyaona hasa ubovu utakao onekana uwekwe wazi wasifiche kama yalivyofichwa mengine.

Comment by Tulonge on February 23, 2013 at 20:28

Hizi tume sometimes huwa hata hazieleweki. Mnakumbuka tume ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi? Report yake ilisaidia nini?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*