Tulonge

Wimbo wa Marijani "Mwanameka" ambao ulitumika kama swali katika mtihani wa kidato cha Nne

Sikiliza tungo za maana za Mwanamuziki wa zamani marehemu Marijan Rajabu katika wimbo wake wa Mwanameka. Kutokna na utaalamu katika kuandika wimbo huo uliojaa ujumbe mzuri, wizara ya elimu ilidiriki kuutumia wimbo huo kutunga swali lililokua katika kipengele cha ushairi katika mtihani wa Kiswahili kidato cha nne mwaka 1990. Ninakumbuka nilikua na mtihani huo ila jitihada zangu za kuutafuta katika kabati langu zimegonga mwamba, nilipenda muone angalau picha ya ukurasa wa swali hilo.

Je wasanii wa muziki wa kizazi cha sasa wanaweza wakaandika tungo zao kwa ufasaha hadi wizara ya elimu ikafanya ilichofanya kwa 'Mwanameka'? Tungo za kina Dully Sykes, Ali Kiba,Mwana FA, Diamond, Professor J, Mzee Yusuph nk zina sifa za kutumika kama swali ktk mitihani ya taifa?

Views: 3990

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on April 4, 2012 at 15:10

Ha haa haa haaaa..... Bonielly umenifurahisha. Ndio huo huo Asimaa. Unazipata wapi? Itabidi tuongee uzuri. Unao kwenye tape au CD? Ama kweli wewe unajua music

Comment by Bonielly on April 4, 2012 at 15:02

hizo zote ninazo mama malaika, hiyo asimaa ooo asimaaa wewe ndie uwa la moyoni mwangu,

Comment by Mama Malaika on April 4, 2012 at 14:53

Bonielly halafu nimesahau Mwenge Jazz band, ilikuwa ya jeshi, sijui bado ipo?

Comment by Mama Malaika on April 4, 2012 at 14:43

Bonielly unakumbuka au umesikia kiba cha Hiba? Hao ni DDC Mlimani Park Orchestra, kibao kinasema Hiiiba imekuwaje mpenzi mbona umebadilika, ninapokuuliza utaki kusema na mimi......

Mie naomba niktafuta Bonielly, ukizingatia niko mbali sina access na Radio One. Ha haa haaa

Una nyimbo za zamani kama vile Karubandika (Marquis du Zaire - Kasaloo Kyanga), Solemba (JUWATA Jazz - Nico Zengekala), Zuwena (Marijani Rajabu), pia Urafiki Jazz vibao vyao; Tausi, Asmaha, Paulina, Safari ya Tanga. Pia huko Tabora nako Nyanyembe Jazz walikuwa na vibao vikali maarafu kama vile Rangi ya Chungwa, Shingo ya Upanga, Asha na vingine vingi nimesahau majina, mzee Segele Matata na wenzie sijui bado mzima?

Ambaye anajua wapi nitapa vibao hivyo na vingine vya band kama vile Jamhuri Jazz, Moro Jazz wana super Volcano na Mbaraka Mwinshehe, Afro Sabini, Les Wanyika, na bands nyingi za kipindi hicho naomba anambie. Bonielly nakupa kazi

Comment by Bonielly on April 4, 2012 at 14:03

mnapozungumzia nyimbo za zamani ujumbe ulienea sana, mnakumbuka mwimbo huu? kumekucha jam kumekucha majogoo vijiji wanawika hata najua mbinguni linatoka wazalendo amkeni? mnaukumbuka na huu? benki ya taifa ya biashara ooo, yahudumia kila mala ooo! ni chombo cha umma kitumieni wananchi,,, mnaukumbuka ngapulila kazamia meri? mnaukumbuka mama maria nyerere kwaheli? mnaukumbuka kriopatra? mnaukumbuka,

kwa wale wapenzi wa nyimbo hizi nawashauri msikilize radio one kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana mtachambuliwa vizuri na mchambuzi wa muziki huo, mpaka utachoka mwenyewe au nitafute nikupatie hizo nyimbo kwa wakati wako kama wewe ni mpenzi wa zilipendwa,

Comment by Mama Malaika on April 1, 2012 at 20:42

Dismas... asante kutuletea blog hii. Umenikuna sana kwa kibao hiki "Mwanameka". Hawa wana muziki wenu wa sasa mwawaita Bongo Flava (sikuwaacha wakati naondoka TZ 1992) niliwahi tumiwa zawadi ya CD na binamu yangu, ilibidi niigawe kwani baadhi ya nyimbo nilikuwa hata sielewi walivyokuwa wanaimba maana hicho kiswahili sijui ndio cha kisasa cha mitaani? Style yao tu kwa ujumla ya uimbaji kwangu haipandi

Comment by jemadari mimi on April 1, 2012 at 14:39

Unajua siku zile watu walikuwa watunzi wa nyimbo zilizojaa mafundisho na busara  nyingi, mfano ebu kasikilize nyimbo ya Orchestra matimila unaoitwa siku ya kufa,acha huu kuna mwimbo wa marijani unaosema mayasa uzuri ni wakuzaliwa nao bila kuwasahau ddc mlimani park na kibao cha uhuru wa zimbambwe jongwe.

kwakweli baba zetu,walifaidi sana kupata burudani halisi kabisa,muziki ulisikika chombo kimoja baada ya kingine,Lkn kwa sasa sioni kama kuna jipya zaidi ya kupiga makelele na kuiga toka kwa hawa waliotangulia,kwahiyo ndio maana hata wasomi wameona watumie miziki yenye ujumbe ,maadili na fasihi zinazoweza kujengewa hoja na wanataluma ili zitumike kufundishia na kuulizwa ktk mitihani yashule zetu hapa bongo.

Tungo za kina dullyskyes,ally kiba,na wengine ni sawa na ubwabwa wa hitma unakuwa na thamani pale tu haujaliwa lkn ukishaliwa tu watu wanasahau kwamba walikula ubwabwa muda fulani,kwahiyo wana uwezo wakufanya nyimbo zao ziweze kutumika kwenye maswali ya mitihani ya wanafunzi wanaomaliza masomo yao ya mwisho.

Comment by Christer on April 1, 2012 at 7:58

Zilipendwa ila bado hot!

Comment by Christer on April 1, 2012 at 7:56

Tehetehetehetehetee @ Dis

Comment by Tulonge on April 1, 2012 at 6:59

Kama vp wauchukue wimbo wa Kingwendu (Mapepe...mapepe..mapepe..) wajaribu kuutungia swali la mtihani wa kidato cha nne.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*