Tulonge

Wizi na ubakaji wahamia Saint John's Dodoma baada ya IFM

Wanachuo wakiwa wameshika mabango ya kushinikiza ulinzi katika chuo cha St. John

Usiku wa kuamkia leo wanafunzi watatu wa chuo cha 'Saint John's' Dodoma walivamiwa na wezi na kuibiwa laptops 3, camera 1,fedha Tsh. 120,000 na hatimaye mmoja wao kubakwa.Wanafunzi hao wamepanga nje ya chuo hicho na wanaishi wasichana pekee katika nyumba hiyo waliopanga.

 

Akizungumza na tulonge.com kwa njia ya simu, afisa uhusiano wa chuo hicho Bw. Karim Meshack amethibitisha tukio hilo kutokea na mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi aliitisha kikao cha dharura. Maamuzi yaliyo fikiwa katika kikao hicho ni pamoja na kuanzisha kituo cha polisi eneo la chuo hicho pamoja na kuweka taa eneo la karibu na chuo hicho kwani kuna giza sana.

 

Kufuatia tukio hili, wanafunzi wa chuo hicho waliamua kufanya maandamano ya amani kuelekea Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma kushinikiza Ulinzi katika chuo hicho.

Views: 401

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*