Tulonge

Zanzibar: Imamu auwawa kwa mapanga shambani kwake

SIKU chache baada ya kutokea kifo cha Padri Evarist Gabriel Mushi kupigwa risasi na watu wasiojulikana kichwani eneo la Beit el Raas, Jana Imamu wa Msikiti wa Mwakaje ameuawa baada ya kupigwa mapanga hadi kufa.


Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hapo jana mchana majira ya saa 8 na kumtaja aliyefariki kuwa ni Sheikh Ali Khamis ambaye ameuawa na watu wasiojulikana.


Kamanda Ahmada alisema Sheikh Khamis mbali ya kuwa ni Imamu wa Msikiti lakini pia ni mkulima na ameuliwa wakati akiwa katika mazingira ya kazi zake ndani ya shamba lake huko Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Akielezea mazingira ya tukio hilo Kamanda Ahmada alisema tukio hilo limetokea baada ya Sheikh Khamis kwenda shambani kwake katika shmba la minazi Kidoti ambapo wakati akiwa shambani hapo ndipo walipotokea watu kadhaa na kumpiga mapanga sehemu za shingoni mwake na kusababisha kifo chake muda mfupi baada ya kipigo hicho.

Alisema baada ya tukio hilo, watu walimchukua na kumkimbiza hospitali lakini kutokana na kupoteza damu nyingi alifariki dunia wakati akiwa njiani na hivyo harakati za mazishi zinafanyika baada ya kuchukuliwa vipimo na wataalamu wa afya.

Kamanda Ahmada ametoa wito kwa wananchi kutopuuzia taarifa za watu ambao wanawashuku na wenye kuleta maafa yakiwemo mauaji hapa nchini, kwani kuwaficha wahalifu ni kuendeleza utamaduni usiofaa katika jamii ambayo imeanza kuharibika kutokana na mauaji hayo yanayoendelea kila kukicha.

Hili ni tukio la nne kwa viongozi wa dini kuhujumiwa ambapo tukio la kwanza Sheikh Fadhil Suleiman Soraga kumwagiwa tindi kali na watu wasiojulikana na kujeruhiwa vibaya wakati akifanya mazoezi nyakati za asubuhi karibu na nyumbani kwake Magomeni, tukio la pili ni lile la Padri Ambrose Mkenda aliyepigwa mapanga shingoni na kurejuhiwa vibaya na watu wasiojulikana wakati akitaka kuingia nyumbani kwake huko Tomondo Mjini Unguja. matukio hayo mawili yalitokea mwaka jana.

Katika mwaka huu nako kumetokea matukio mawili kwa kuuawa kwa Pardi Evarist Mushi huko Beit El Raas wakati akitaka kuingia Kanisani na pia kuuawa kwa Sheikh Ali Khamis huko Kidoti shambani kwake Mkoa wa Kaskanizini Unguja. Inna lillahi wainna ilayhi rajiiun.

Chanzo: saidpowa.blogspot.com

Views: 799

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by David Edson Mayanga on February 25, 2013 at 13:30

mh kumekucha tena huko kama kawaida yao

Comment by Dixon Kaishozi on February 25, 2013 at 12:07

                                       ............... Speechless .............

Mungu Tunakuomba Utusaidie. Amen!

Comment by Mjata Daffa on February 25, 2013 at 8:45

Wadau tuchangie hoja kama watu walioenda shule, kusema shekh wenu huyo utakuwa hutafutiani na watu waliibeba dhambi ya ubaguzi nakuomba kama cha kusema kaa kimya usichee ubaguzi wakidini.

Binafsi maoni yangu hoja ya udini haipo ispokuwa kunawatu wanamaslahi na vita ya wenyewe kwa wenyewe hapa kuna mkono wa mataifa ya magharibi walifanikiwa Burundi, Randwa na Kongo sasa wanakuja TZ be very careful hawajamaa wanaka kuuza siraha kwa madini, mafuta na GESI iliyogunduliwa hivi karibuni, tunachunguze sana haya makampuni makubwa kutoka marekani na kwengineko yaliyopo TZ kwa kivuli cha kutafiti Nishati za mafuta na GASI. Watanzania tusiwe mambumbu huu mchezo mchafu unatokawapi? kwanini wauwawe viongozi wa dini tu? Walianza na wakristo wakaona hakuna reaction sasa wamehamia kwa waislam nawaomba waislamu nao wawapuuze kama walivyofanya wakristo. Serikali lazima iwajibike kwa kuzitambua hizo njama chafu

Comment by Christer on February 25, 2013 at 8:36

Watu wasiojulikana? manake nn? Tuna macho lakini hatuoni, tuna masikio lakini hatusikii. Kweli kbs Mgao kila siku ni viongozi wa dini, alaf inaitwa vita ya watu wasiojulikana!!! hao watu wasiojulkana mbona hawauwi viongozi wa serikali? au hawauwi viongozi wa makampuni ya sector binafsi na ma NGO'S? Kweli haihitaji tuition @ Lyehagi mwenye kuelewa na aelewe mbishi na aendelee kubisha. Tzania tusipokua makini, tutakua km nchi za wenzetu zenye vita ya wao kwa wao, Watanzania tunatakiwa tumuogope Mungu na tumuombe Mungu aturehemu sawasawa na mapenzi yake kwetu, hasa ktk kipindi hiki cha kumwagika kwa damu za viongozi wetu.

Comment by Christer on February 25, 2013 at 8:33

Watu wasiojulikana? manake nn? Tuna macho lakini hatuoni, tuna masikio lakini hatusikii. Kweli kbs Mgao kila siku ni viongozi wa dini, alaf mnataka kusema hii ni vita ya watu wasiojulikana!!! hao watu wasiojulkana mbona hawauwi viongozi wa serikali? au hawauwi viongozi wa makampuni ya sector binafsi na ma NGO'S? Kweli haihitaji tuition @ Lyehagi mwenye kuelewa na aelewe mbishi na aendelee kubisha. Tzania tusipokua makini, tutakua km nchi za wenzetu zenye vita ya wao kwa wao, Watanzania tunatakiwa umuogope Mungu na tumuombe Mungu aturehemu sawasawa na mapenzi yake kwetu.

Comment by Lyehagi Mazuli Mhuli Jr. on February 24, 2013 at 19:55

Haya ndo mlokuwa mnayataka na shekhe wenu huyo, haya yamalizeni sasa...

Chalii huwezi kuhitaji tuition ili upate majawabu ya hilo.. YANATIA KINYAA....

Comment by Mama Malaika on February 24, 2013 at 16:28
Uwiii! Sirikali inafanya nini jamani viongozi wa dini wanaendelea tolewa roho? Na kwanini kupigwa na kuuawa viongozi wa dini we visiwani siku zote? Hawa ndugu zetu wa nini?
Comment by Omary on February 24, 2013 at 0:33

Hapa bila MUNGU kuweka mkono wake watu watamalizana MUNGU tunusuru na hii vita ya wenyewe kwa wenyewe watanzania tunauwana wenyewe sasa huu udini unatoka wapi? maana TZ leo ukiangalia mama mkiristo baba muislam utamuuwa nani? umuache nani? na kwa nini tuuwane? kama kuna tatizo tukae chini tuongee tulitatuwe na sio kuuwana kama wanyama watu hawana woga na MUNGU yaani ubinadam umetoweka kabisaa sijui tunaelekea wapi?! MUNGU mwenyewe ndio anajuwa.

Comment by MGAO SIAMINI,P on February 23, 2013 at 23:26

@chalii hapo haitaki degree ya aina yeyote wala elimu ya utafiti,labda kuwatafuta wauwaji ndo itahitaji weredi haya mauaji yana uhusiaono chanya na dini mbona hatusikii mvuvi au mfanyabiashara au mfanyakazi ila madhumuni ya mauaji ndo ngumu kuzungumzia.ngoja tusubiri uone majibu si tumesikia serikali imekopa ma FBI wanafanya kazi badala ya usalama wa taifa na polisi wetu tunatia huruma.

Comment by ILYA on February 23, 2013 at 23:10

How do you judge?!.How terrible is your Judgment ?!.

Hapo sasa,habari inasema:Imam huyo kauliwa na watu wasiojulikana:Nani anaweza kutwambia hapa kuwa hao watu wasiojulikana waliotenda jinai hiyo ni wakristo?!.Habari iliyopita ya kuuliwa kwa Padri Evarist Gabriel Mushi ilikatiza mtaa huu na baadhi ya wadau wakasema:WATU HAO (WASIOJULIKANA)waliomwaga damu hiyo ya padri huyo ni waislaam!!.Itakuwa ni haki ya kila mtu kuuliza maswali kama haya:

What is the matter with you?!.How terrible is your Judgment?!.How do you judge?!.

Na IL-YA

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*