Tulonge

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameingia matatani, baada ya kutakiwa kukanusha tuhuma alizozitoa bungeni katika Mkutano wa Tisa wa Bunge, kwamba mfanyabiashara wa kigeni, Moto Mabanga, alipewa vitalu vya mafuta kinyume na taratibu.

Mfanyabiashara huyo amesema kuwa iwapo Zitto atashindwa kukanusha tuhuma hizo, atafikishwa mahakamani.

Barua iliyoandikwa kwenda kwa mbunge huyo iliyosainiwa na Mwanasheria wa Mabanga, Lawley Shein wa Kampuni ya Uwakili ya Lawley Shein Attorneys, ambayo Mwananchi Jumapili limeiona, inaeleza kuwa hoja binafsi aliyoitoa Zitto, haikuwa na ukweli wowote.

Barua hiyo ya tarehe 28 Novemba, 2012 ilisema kuwa hoja hiyo ya Zitto ni ya uongo, imemkashifu mteja wao na kumshushia hadhi yake binafsi na biashara zake.

“Katika kuthibitisha kuwa tuhuma zako siyo za kweli katika hoja uliyotoa, umemtaja mteja wetu kama raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mteja wetu ni raia wa Afrika Kusini, lakini, umeamua kumtaja kama raia wa Kongo bila kuangalia ukweli,” alisema Shein.

Katika barua hiyo, Shein pia amesema kuwa Zitto amemtuhumu mteja wake Mabanga kuwa aliwahonga baadhi ya vigogo serikalini na kuwapa rushwa wanasiasa katika mchakato wa kufanikisha upatikanaji wa vitalu hivyo.

“Tuhuma hizo siyo za kweli, mteja wetu alifuata taratibu zote kwa uwazi na mamlaka husika nchini na hakuwahi kutoa rushwa kwa mtu yeyote,” alisema mwanasheria huyo.

“Tuhuma hizi ni za uongo, zimemharibia jina mteja wetu na kumsababishia madhara. Kama hutazifuta kauli hizo, uongo huo utamsababishia mteja wetu madhara makubwa zaidi na tutalazimika kudai fidia,” Shein alionya kupitia barua hiyo.

Shein aliongeza kuwa pamoja na Zitto kuongea hoja hiyo akiwa bungeni hivyo kuwa na kinga ya kibunge, lakini kwa mazingira aliyotolea hoja hiyo alitumia vibaya kinga ya kibunge, anayopata mbunge yeyote anapotoa hoja akiwa bungeni.

Kupitia barua hiyo, Shein alimtaka Zitto kufuta kauli yake dhidi ya mteja wao na kwamba mteja wao ana haki zote za kushtaki dhidi ya hoja hiyo.

Zitto azungumza
Alipotakiwa kuzungumzia hoja hiyo na hatua atakazochukua, Zitto alisema kuwa amemwandikia barua Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, kumjulisha hatua hiyo ya kutaka kushtakiwa.


“Nimemwandikia Katibu wa Bunge kumjulisha kwamba nimeletewa kusudio la kushtakiwa, maana hili ni suala la Kinga ya Bunge,” alisema Zitto na kuongeza:

“Mbunge ana kinga kwa masuala aliyozungumza ndani ya Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 100 ya Katiba. Kwa hiyo Katibu (Dk Kashililah), atawajibu hao wanasheria.”

Ibara hiyo ya 100 (2) inaeleza kuwa; Bila ya kuathiri Katiba au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo alilosema au kulifanya ndani ya Bunge, au alilolileta bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.

Naibu Spika
Kwa upande wake Naibu Spika, Job Ndugai alisema kuwa hana taarifa za kusudio hilo la kutaka kushtakiwa kwa Zi tto, lakini akasema kwamba mbunge ana kinga ya Bunge pindi akitoa hoja au wazo lolote, akiwa ndani ya Bunge.

Ndugai alisema kuwa kutokana na mabadiliko madogo ya sheria yaliyofanyika, mwananchi anaweza kuandika barua kwa Spika wa Bunge kutokana na tuhuma alizotoa mbunge dhidi yake bungeni.
“Mtu anaweza kuandika barua kwa Spika na Spika ataona hatua zaidi za kuchukua za kibunge,” alisema Ndugai.

Chanzo: mwananchi.co.tz

Views: 452

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on January 18, 2013 at 10:40

unajua nini@ mama, maviongozi yetu yananjaa na uchu wa madaraka,ulimbikizaji wa mali na hayajiamini yakikutana na muwekezaji akayanunulia wisky utashangaa maongezi unaweza kupigana utafikiri wanazungumzia mali ya familia yake.niliwahi kuwa jirani hoterini na mpumbavu anaejiita mheshimiwa na mtu aliejitambulisha kama mwekezaji,hajui kitu yaani ni yes sir;no problem sir nusu ningilie

Comment by Mama Malaika on January 17, 2013 at 10:30
na hili suala la uraia sio tija, watu tuna uraia wa nchi ulozaliwa, nchi walozaliwa wazazi wako, nchi unayoishi makazi, na pia nchi ulo oa au kuolewa. Hivyo ukute huyo mfanya biashara ana uzaire na kumiliki passports nyingi
Comment by Mama Malaika on January 17, 2013 at 10:11
ukiona mikataba inafichwa kiasi hicho jua kuna corruption ndani yake kwani hizo natural resources ni mali ya watanzania wote hivyo mikataba ipitishwe bungeni.
Na huyu Zito sio kichaa, hawezi tu kuropoka kitu lazima kuna ukweli ndani
Comment by Dixon Kaishozi on January 17, 2013 at 9:03

Mama Malaika, swala la mikataba nchii hii ni siri kubwa sana.. Kuna mbunge mmoja nilimuona kwenye tv flan hapa akisema.. "ukitaka kuona mkataba wowote ule.. kwanza unapewa ulinzi ambaye atakusimamia wakati unausoma mkataba huo, huruhusiwi kuunakili, kutoa kopi au kufanya kitu chochote, unausoma na kuuacha hapo hapo" . Swali ni kwamba kwanini inafichwa kiasi hicho? isiwe wazi wa wananchi wote ? ndo hali alisi.

Comment by Lyehagi Mazuli Mhuli Jr. on January 14, 2013 at 20:52

Huyu tajiri anauhakika na kile anachosema au ndo yle yale ya mafisadi na kusafishana? Mbona ishu yenyewe ya siku kibao alikuwa wapi? Au mpaka amefanya mawasiliano ya wahusika wa uchakachuaji ili alindwe vizuri?

Comment by Mama Malaika on January 14, 2013 at 17:38

Kuikoa nchi toka kwa wawekezaji matapeli wa kimataifa hasa kwenye natural resources inapasa sirikali ya Tanzania kufanya maombi ya mikataba yote ya wawekezaji toka nje yawe transparency, tena maombi yapitie bungeni na kuchunguzwa kabla foreign investor hajapewa kibali. Huwezi ingia Britain as a foreign investors ukapewa kibali bila kupitishwa na wabunge, watataka wakujue tabia huko ulikotoka na sifa za biashara unayodhamiria. Na ndio maana matapeli wawekezaji wanakimbilia Africa hasa hasa Tanzania ambayo imegeuzwa kichaka cha wendawazimu, wageni wanakuja kupitia milango ya nyuma wanapewa wanavyotaka na kuondoka kupitia milango ya nyuma kwa upumbafu wa wa watu wachache sirikalini.

Comment by william massawe on January 14, 2013 at 9:54

NO RESERCH NO RIGHT TO SPEAK!!!!sawa mheshimiwa ZITTO KABWE!!!{unaongea vi2 wenyewe wakimaind unakimblia kinga ya bunge why????!!!---usiwaogope kama unajiamini waache waende huko mahakamani!}

Comment by Dixon Kaishozi on January 14, 2013 at 8:44

Hizi porojo tu.. Kama umekosewa unasubiri nini kwenda mahakamani ?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*